Tanzania: Utifuaji mdogo wa udongo unawalipa wakulima wa mtama na uwele

| Juni 19, 2017

Download this story

Susan Mathias hakumbuki vizuri mara ya mwisho familia yake ya watu saba imekaa njaa. Lakini mvua zisizotarajiwa na gharama kubwa ya ukulima imeathiri mavuno yake.

Ni Mama wa miaka 36 anaishi kijiji Mchemwa, jirani na Dodoma, mji mkuu wa Tanzania. Anamiliki zaidi ya hekari 40 ya ardhi ya uzalishaji akizalisha mazao kama mahindi, uwele, mtama na mboga mboga.

Kilimo ni uti wa mgongo kwenye uchumi wa mkoa, ingawa ukame unaathiri kilimo. Mbadiliko ya hali ya hewa na ardhi isiyo na rutuba imeathiri uzalishaji kwenye eneo.

Mavuno ya Uwele wa Bibi Mathias kwa mfano, yamepungua kutoka magunia matano hadi magunia mawili kwa hekari moja katika miaka ya 2000. Amesema kikwazo kubwa ni kupuuzia, akielezea zaidi ukosefu wa maarifa kuhusu kulinda rutuba ya udongo. Amesema ,Mashamba yangu mengi yalikuwa makavu, hayakuweza kutunza unyevunyevu kwa muda mrefu baada ya mvua.

Bibi. Mathias alishiriki kwenye mafunzo yaliyoendeshwa na Dayosisi ya central Tanganyika. Kupitia hayo mafunzo, alijifunza kuhusu kilimo hifadhi, kilimo ambacho kinalinda udongo kwa kupunguza utifuaji na shughuli zingine zinazoharibu udongo.
Kilimo hifadhi inalinda udongo kwa kuzuia mmomonyoko na uchakavu, inaongeza ubora wa udongo na kuchangia kwenye uhifadhi wa mali asili huku ukiongeza mavuno.

Tangu apate mafunzo, bibi Mathias anaandaa shamba lake kwa kutumia futi, kamba, panga na majivu badala ya trekta na jembe la wanyamakazi.

Anagawanya ardhi yake ndani ya mashamba madogo yenye mita mraba 20. Kwa njia hii inakuwa rahisi kufanya mzunguko wa mazao baina mashamba haya.

Kisha Bi. Mathias anatifua udongo kidogo, akiacha magugu na masalia ya mazao juu ya ardhi. Anatumia haya kufunika udongo, ambayo yanazuia mmonyoko wa ardhi unaosababishwa na mvua na upepo na inatunza unyevunyevu kwenye udongo.

Akiwa anaotesha, anatifua mashimo la usawa mmoja, ambayo huwa angalau kina cha sentimita 15. Baada ya shamba kuwa tayari, anaongeza kijiko cha chai cha majivu katika shimo la kupandia, ikifwatiwa na udongo kidogo na kijiko cha chai cha mboji. Baada ya hapo anaongeza udongo kidogo katika shimo, anapanda mbegu kisha anaongeza udongo zaidi na kuacha kina kifupi.

Majivu yanasaidia kupunguza tindikali kwenye udongo na kulinda dhidi ya mchwa ambao wanaathiri mimea. Kina kifupi kinahifadhi maji ya mvua kwa ajili ya ukuaji wa mmea.

Wakulima wa wilaya ya Dodoma pia wanapanda mazao funika, ambayo ni njia nyingine ya kilimo hifadhi. Wanachanganya mtama au ulezi na mazao funika ambayo inazuia magugu na kuongeza virutubisho kwenye udongo.

Jamii ya kunde hutumika sana kama mazao funika wakulima kama Bibi Mathias wapanda mazao jamii ya kunde kama kunde, mbaazi, lablab, choroko na jack bean kama mazao funika.

Samweli Elinuru ni afisa ugani wa wilaya ya Dodoma. Anahamasisha Kilimo hifadhi katika vijiji sita. Amesema kuwa idadi ya wakulima wanaofanya kilimo hifadhi kwenye hili eneo imeongezeka kutoka 62 mwaka 2005 hadi 850 kwa msimu huu.

Anaongeza, “Wakulima wanafurahia kwa sababu wakitumia mazao funika, wanapata pia mazao ya ziada kwa ajili ya chakula na kuuza.”

Lawrence Lwanji ni afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Dayosisi ya Central Tanganyika, ambayo inawafunza wakulima juu ya kilimo hifadhi. Amesema,”wakulima wanaonyesha kupenda kutumia kilimo hifadhi. Tunapokea simu nyingi kutoka maeneo ambayo bado hatujafika……wanahitaji elimu hiyo ili kubadili njia zao za kilimo.

Donald Mangwela ni mkulima katika kijiji cha Chihanga. Anasema sababu muhimu ya kufanya kilimo hifadhi ni kwamba ina gharama ndogo. Bw. Mangwela anaelezea: “Kwenye kilimo cha kawaida tunatumia trekta, power tiller au plau, ni gharama zaidi ya kilimo hifadhi, ambayo tunatumia tu masalia ya mazao kuzuia magugu. Hata kwenye eneo dogo la shamba, tunakuwa na uhakika wa kupata mazao zaidi.”

Hata hivyo, anasema, “Kwa wanaoanza kuwekeza kwenye kilimo hifadhi wanahitaji maandalizi ya mapema ili kuepukana na uharakishaji dakika za mwisho.” Hii ni kwa sababu wanaonza wanahitaji muda mwingi kuondoa magugu na kujifunza mbinu mpya ya kilimo. Lakini bw. Elinuru anasema ni vyema kutia bidii kwani kilimo hifadhi kina gharama ndogo kuliko mbinu za kilimo cha kawaida.

Kama ukiangalia kwa haraka unaweza kuona tofauti. Mazao yaliyooteshwa kwa njia ya utifuaji mdogo wa udongo yamerefuka na yenye afya kuliko yale yaliyooteshwa kwa njia za kilimo cha kawaida.

Photo: Donald Mangwela in his field

This work was created with the support of Canadian Foodgrains Bank as part of the project, “Conservation Agriculture for building resilience, a climate smart agriculture approach.” This work is funded by the Government of Canada, through Global Affairs Canada, www.international.gc.ca