Utangulizi: Ufugaji wa Mbuzi

| Novemba 20, 2018

Download this story

Kwa nini somo hili ni muhimu kwa wasikilizaji?

Kwa sababu wakulima ambao wanataka kuongeza mbuzi wanapaswa kujua:

– Umri sahihi na uzito kwa ajili ya mbuzi kuanza uzalishaji na msimu bora wa upandishaji.
– Mbinu bora za uzalishaji.
– Dalili za magonjwa ya mbuzi na maambukizi.
– Jinsi ya kutunza mbuzi wajawazito pamoja na watoto kabla na baada ya mbuzi kuzaa.
– Kiasi cha chakula na maji kinachohitajika kwa siku kwajili ya malisho ya mbuzi
– Namna bora ya kulisha mbuzi ili kuongeza zaidi kipato na faida kutoka kwa masoko.

Vipi ni vidokezo muhimu?

– Kwa asili mbuzi ni watafutaji binafsi wazuri wa malisho. Mbinu bora ya ulishaji wa mbuzi ni kuhakikisha wanapata malisho mazuri kwasababu afya na ukuaji wa mbuzi hudorora kwa ufugaji wa ndani.
– Mbuzi wanapaswa kulishwa mara tatu kila siku, na maji yakipatikana wakati wote.
– Vifo vya mbuzi wadogo kwa ujumla vipo juu sana. Wafugaji wa mbuzi wanahitaji kuwa makini hasa katika utunzaji wa hao mbuzi wadogo.
– Mbuzi wenye afya dhaifu wanapaswa kutengwa na wale wenye afya imara.
– Mbuzi wanapaswa kupandishwa pale tu ambapo kuna vyakula vya kutosha vyenye asili ya protini.
– Baada ya kuzaliwa tu, watoto wa mbuzi wanapaswa kunyonya maziwa ya mama kwa takribani muda wa dakika 20 mpaka 30.
– Maziwa huwa na harufu mbaya kama mbuzi atalishwa kwenye malisho yenye harufu au kama mbuzi jike hutunzwa pamoja na mabeberu.

Je, zipi ni changamoto kubwa za ukuzaji wa mbuzi?
– Kutambua magonjwa na dalili ambazo hazionekani kwa urahisi.
– Kujua wakati sahihi wa upandishaji wa mbuzi.
– Kutokujua mchanganyiko sahihi wa chakula bora chenye virutubisho sahihi
– Ukosefu wa maarifa ya upandishaji sahihi.

http://scripts.farmradio.fm/sw/radio-resource-packs/kifurushi-namba-106/utangulizi-ufugaji-wa-mbuzi/