Jinsi ya kuandaa kipindi kizuri kuhusu masoko na matangazo

| Oktoba 3, 2018

Download this story

Kipindi cha masoko na Matangazo ya masoko ni kipindi cha aina gani?

Kipindi cha redio cha masoko kinatoa taarifa za masoko na kuunganisha wakulima na wadau wengine wa masoko. Kipindi kinatoa huduma za taarifa za masoko kwa Wakulima ambazo taarifa hizi zinaongeza fursa za masoko na kuongeza kipato.

Inawezaje kunisaidia mimikumhudumia msikilizaji vizuri?

– Inamsaidia mkulima kupata bei nzuri ya mazao yake sokoni kwa kumsambazia mkulima taarifa za masoko kwa wakati na kumsaidia mkulima masoko ambayo anaweza kuuza mazao yake.
– Inamsaidia mkulima kuchagua aina gani ya mazao anayopaswa kupanda, kulingana na bei ya masoko na gaharama za uzalishaji.
– Inamjengea mkulima uwezo na ujasiri wa kuweza kufanya makubaliano na wanunuzi.
– Inamsaidia mkulima kujifunza mahusiano na wadau mbali mbali wa masoko na kuboresha uhusiano.
– Inatoa uwanja kwa wadau mbali mbali wa masoko kukutana pamoja na kukubaliana juu ya bei za mazao kulingana na changamoto zilizokuwepo.
– Inamsaidia mkulima kuweza kujua anapaswa kutoza kiasi gani cha fedha kwa mavuno yake ili kupata faida.

Nina anzaje? (Jifunze zaidi katika kipengele cha maelezo hapa chini.)

1. Wajue Wadau wa Masoko.
2. Angalia nguzo kuu nne za Masoko (Bei, Bidhaa, Promosheni na Eneo ).
3. Nitumie muundo gani katika kipindi cha masoko?
4. Tumia TEHAMA na simu za mkononi kuboresha kipindi chako cha masoko.
5. Mada za kujadili katika kipindi cha masoko.
6. Ni muda gani au msimu gani wa kurusha kipindi cha masoko?
7. Changamoto za kuendesha kipindi cha Masoko.

http://scripts.farmradio.fm/sw/radio-resource-packs/kifurushi-namba-108/jinsi-ya-kuandaa-kipindi-kizuri-kuhusu-masoko-na-matangazo/