• enEnglish
  • frFrançais
  • ptPortuguese
  • swSwahili
  • amAmharic
  • haHausa
  • Stories
  • Resources
  • Script of the week
  • Opportunities
  • Spotlights
  • FRI in Action
  • This story is also available in English
  • This story is also available in Français

Tanzania: Wakulima walima maharage ya Canavalia kama zao funika kuboresha rutuba ya udongo

Method Charles | Mei 24, 2018

conservation-agriculture-sw swahili-post_tag

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

Download this story

Shamba la Happy Mafie laonekana kuwa na ukijani mzuri na lilio tunzwa vizuri. Maharage ya Canavalia yanafunika ardhi vizuri kiasi ya kwamba jua kali linashindwa kufyonza unyevu wa ardhi, na kipindi cha mvua udongo haumomojnyoki. Analima kilimo hifadhi, anaotesha maharage ya Canavalia katika eneo kubwa la shamba lake, maharage haya yanasaidia kufunika udongo katika shamba lake.
 
Bi. Mafie anatokea katika kijiji cha Njeku wilaya ya Arumeru kasakazini mwa Tanzania. Yeye na mume wake wanalima ndizi na kahawa katika maeneo ya mteremko chini ya Mlima Meru. Pia wanalima pilipili, spinachi, vanilla, papai na matunda pasheni. Baada ya kuvuna huwa anapanda mharage ya Canavalia. Pia anafanya kilimo mseto cha maharage na mahindi.
 
Anaelezea,“Tulianza na kilo 10 za maharage ya Canavalia lakini sasa tuna magunia 100 [60-kg]. [Ya maharage] imetusaidia kuvuna mahindi na ndizi.”
 
Bi. Mafie anasema maharage ya Canavalia ni mazao yanayoongeza kiwango cha naitrojeni kwenye ardhi. Pia inafunika ardhi, inatunza unyevu na kupunguza mmomonyoko. Kulingana na Bi. Mafie, hii inamaanisha sikuzote anapata mavuno mazuri ya mahindi, hata kipindi cha kiangazi kibaya.
 
Alijufunza kupanda maharage ya Canavalia kutoka kampuni ya East Africa Impact Center. Afisa ugani Charles Boniventure alipomtembelea Bi. Mafie, alimshauri atumie mboji au mazao funika kulinda udongo wake. Anasema, “Kupanda maharage ya Canavalia katikati ya zao lolote ni vizuri kwani llinaongeza rutuba ya udongo ambayo inasaidia zao kukua haraka.”
 
Bw. Boniventure anaongeza, “Tumejitahidi kuongeza upandaji wa maharage ya Canavalia, ambapo imetusaidia kwasababu kwanzia tuanze kupanda mazao yameongezeka kulinganisha na miaka mingine.”
Afisa ugani alimpatia Bi. Mafie gunia moja la mbegu ya maharage ya Canavalia amabyo alipanda baada ya kupanda mahindi yake.
 
Sasa anatengeneza hela nzuri kwa kuuza maharage ya Canavalia kwa wakulima wengine, ambao wanatumia kama chakula au mbegu. Anaongeza, “Tunauza kilo moja ya Canavalia kwa shilingi 15,000 [sawa na dola 6.50].”
 
Wakulima wengine na maafisa ugani wanatembela shamba la Bi. Mafie’s kujifunza jinsi anavyolima tumia maharage ya Canavalia kufanya kilimo hifadhi.
 
Anatumaini kuwa wakulima wengine katika eneo lake wataanza kulima Canavalia. Anasema familia yake itaendelea kuangalia namna ya kutumia Canavalia kuendeleza kilimo.
 
Hii imetengenezwa kwa msaada wa Canadian Foodgrains Bank kama sehemu ya mradi, “Kilimo hifadhi kujenga ujasili, kilimo bunifu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya nchi.” Kazi hii imefadhiliwa na serikali ya Canada, kupitia Global Affairs Canada, www.international.gc.ca.

Related

About Barza Wire

Barza Wire is a service of Farm Radio International.
This news service shares stories about rural communities in Africa. Our content is available for use by radio broadcasters. Sign up for the newsletter.


Contact Us

Farm Radio International
1404 Scott Street
Ottawa, Ontario
Canada, K1Y 4M8

Tel: 1.613.761.3650
Fax: 1.613.798.0990
Toll-Free: 1.888.773.7717
Email: barza.fm@farmradio.o

© 2026 Farm Radio International