Tanzania: Pembejeo za kilimo zimesaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa soya

| Juni 19, 2017

Download this story

Daniel Lungo ni mkulima mdogo ambaye analima soya kijiji cha Utiga Mkoani Njombe nyanda za juu kusini mwa Tanzania, eneo lenye hewa ya baridi na udongo wa kichanga.

Bw. Lungo ni baba wa watoto watano, ambaye amekuwa akilima soya kwa miaka mitatu mfululizo kwenye shamba lenye ukubwa wa nusu hekari. Anasema mwaka 2016 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwake kutokana na kuweza kuvuna mazao mengi ukilinganisha na miaka iliyopita.

Bw. Lungo anasema haya yaliwezekana kutokana na mbinu mpya za kilimo ikiwemo matumizi ya mbolea na inoculant. Mr Lungo huandaa shamba lake kwa jembe la ng’ombe. Kisha huchanganya mbegu za soya na inoculant ambayo ina bacteria aina ya Rhizobia wanaoongeza nitrojeni kwenye udongo.

Mbali na hiyo, Bw. Lungo anatumia pia mbolea aina ya DAP wakati wa kupanda na baada ya kupalilia ambapo inasaidia soya kukua kwa haraka ingawa anasema ni gharama sana “Tunanunua kg 50 ya mbolea kwa sh60,000 ambayo ni sawa na dola 26 za kimarekani jambo ambalo mkulima wakawaida hawezi kuhimili, wachache ndio wanaweza.”

Anasema baadhi ya wakulima wanaweza kumudu gharama lakini ni gharama mno kwa wengine. Mbolea inagharimu sh 30,000 mbazo ni sawa na dola 13 za kimarekani lakini mkulima huyohuyo haruhusiwi kupata zaidi ya kg 50 za mbolea ambayo kitaalamu inatumika kwenye shamba la heka moja tu. Na vilevile kiwango kinahotolewa cha pembejeo za ruzuku ni kidogo jambo linalochangia wakulima wengine kukosa pembejeo hizo.

Wakati ambapo soya ni jamii ya mikunde inayoongeza rutuba ya udongo, Bw. Lungo anasema mbolea inamsaidia mkulima kupata mavuno mazuri “Eneo letu lina udongo wa kichanga ambao unahitaji mbolea wakati wa kupanda na baada ya kupalilia bila hivyo huwezi kupata mavuno mengi.”

Wakati wakulima wa Tanzania wanapata kiwango kidogo cha mbolea ya ruzuku, Bw. Geoffrey Kirenga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu (CEO) wa mpango wa kukuza kilimo nyanda za juu kusini (SAGCOT) anasema kuwa mpango huu wa serikali wa kusambaza pembejeo za kilimo una faida zake pia ikiwemo kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya matumizi ya mbolea za zana za kisasa za kilimo ingawa bado ni kwa kusuasua.

Alifanunua kuwa, mpango huu ulianza mwaka 2003 ambapo wakulima wa Tanzania alikuwa chini ya tani 100,000 ya mbolea kwa mwaka lakini hali ilivyo kwa sasa kiwango kimepanda hadi kufikia tani 300,000 ingawa Bw. Kirenga anasema bado ni kiwango sana. Aliongeza kuwa “Yapo mengi ya kuongezwa na kuboreshwakwenye sekta ya kilimo ikiwemo upimaji wa udongo kuhakikisha tunatumia kile ambacho tunakihitaji kwani inasaidia kutotumia fedha vibaya ikiwemo kutunza mazingira.”

Mkulima mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Frank Mwagike toka kijiji cha Wanging’ombe amekuwa akilima maharage ya soya kwa zaidi ya miaka 15 akitumia mbegu za asili bila kutumia mbolea ama madawa ya kuulia wadudu kilimo ambacho alikuwa akikifanya kwa ajili ya matumizi ya nyumbani tu kutokana na uhaba wa soko.

Kwa sasa analima eneo la ukubwa wa robo tatu heka akitumia pembejeo za kilimo kuongeza uzalishaji. Kwa sasa anatumia mbolea ya kiwandani mara mbili kwa mzimu wakati wa kupanda na baada ya kupalilia. Na anabainisha kuwa hii ni kutokana na msaada alioupata kutoka shirika la Farm Input Promotions Africa lilipo mkoa wa Njombe.

Deo Msemwa ambaye ni meneja wa shirika hilo “ Tunachokifanya sisi ni kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo kama vile mbegu na mbolea.”

Bw. Msemwa anabaiisha kuwa, aina hii ya mbegu ya maharage inayojulikana na jina la “Quality declared seeds” imetengenezwa na wakulima kwa uangalizi wa taasisi ya Tanzania Official Seed Certification Institute ambayo imethibitishwa kufaa kuuzwa.
Bw. Lungo amekiri kuwepo na ubora wa mbegu hii ambapo anasema inazaa sana na inavumilia magonjwa.

Wakulima wa Njombe wamekabiliwa na mabadiliko ya Tabia nchi kwa mwaka huu. Wakulima hutegemea kupanda maharage kipinid cha mwezi wa kwanza wanzoni ila iliwapasa kusubiri hadi mwezi wa pili kwa kutokana na kukosekana kwa mvua ingawa afisa ugani wa wa kijiji Cha Mwangin’ombe bado anaamini kuwa wakulima wa maharage watavuna vizuri mazao yao.

Bw. Msemwa aliongeza kuwa “Pembejeo hizi za kilimo ni za muhimu kwa sababu zinasaidia mazao kustahimili ukame na magonjwa na hasa kama mkulima atatumia vizuri kama inavyoelekezwa upo uwezekano mkubwa wa kuvuna mazao mengi hata kama kuna mabadiliko ya tabia nchi.”

This work was carried out with the aid of a grant from the International Development Research Centre, Ottawa, Canada, www.idrc.ca, and with financial support from the Government of Canada, provided through Global Affairs Canada, www.international.gc.ca

Photo credit: H. Zell