Tanzania:  Mkulima mdogo ajitengenezea ajira kwa kuanzisha kilimo cha biashara cha maharage

| Juni 19, 2017

Download this story

oram Elia akiwa katika shamba lake la maharage, mkono mmoja akiwa amebeba jembe na mkono mwingine akiwa ameshika Daftari na kalamu kwaajili ya kunukuu dondoo zake.Kwa misimu miwili sasa Joram na marafiki zake wamekuwa wakilima maharage. Anasema, “Hii ndio sehemu yangu ya maisha ya kila siku, siku zote ninahakikisha kuwa shamba letu la maharage lina hudumiwa na wenzangu wanaendelea vizuri na shughuli nyinginezo.”

Kijana mwenye miaka 27 anaishi Sakina, Sakina ni mji mdogo uliopo umbali wa kilometa saba kaskazini magharibi mwa mji wa Arusha kaskazini mwa Tanzania. Joram anasafiri kila siku kuhudumia shamba la nusu ekari la maharage lililopo kijiji cha  Arcedo, kilichopo kama kilometa sita Kaskazini Mashariki mwa Arusha.

Baada ya miaka minne ya jitihada za kutafuta kazi bila mafanikio Bwana Elia na marafiki zake waliona fursa katika kilimo na walianza kujihusisha na shughuli za kilimo, walianzisha kikundi kiitwacho, Keranyi Youth Development Group. Shughuli zao kubwa ni kilimo lakini pia wanajihusisha na utalii na sanaa. Bw. Elia anaeleza, “ Tumechagua kilimo kama shughuli kuu kwasababu kuna fursa kubwa katika kilimo biashara na hapa tuna mazingira tayari kwa kufanya kilimo hapa.”

Anaongeza, “Kufanya kazi katika kikundi inatuweka katika nafasi nzuri ya kuweza kupata mikopo na mafunzo ya kitaalamu kutoka serikalini na mashirika binafsi ila kufanya kazi mwenyewe ni vigumu kupata vitu hivi.” Kikundi kimepata mikopo miwili mikubwa ambayo imewawezesha kuboresha utendaji wao: Silingi milioni tatu za kitanzania kutoka serikali ya Tanzania na shillingi laki nne kutoka katika shirika binafsi liitwalo  Vision for Youth. Lazima walipe mikopo yao yote, watalazimika kulipa riba ya asilimia 25 kwa mkopo wa waliopewa na Vision for Youth.

Kikundi hiki pia kimepatiwa mafunzo mabilimbali na shirika la Vision for Youth juu ya mada kama kuandika mpango kazi na namna ya kuwasilisha na kuelezea mada. Bw. Elia anasema, “Kilimo biashara ni fursa nzuri kwa vijana wasio na ajira. Ninatazama kilimo biashara kama biashara nyinginezo zenye mafanikio tjough it is not easy there are lots of challenges.”

Changamoto ya kwanza ilikuwa kupata ardhi na nyingine ilikuwa ni kutafuta fedha ya kulipia shamba na changamoto ya tatu ilikuwa ni mvua kidogo zilizo pelekea kukauka kwa miferegi ya kunyeshea lakini changamoto kubwa ilikuiwa ni ukosefu wa elimu jinsi ya kupanda maharage.
 
Kwa msimu wa kwanza mwaka uliopita  walitegemea kuvuna kilo 800 mpaka kilo  1,000 za maharage lakini walipoteza karibia mavuno yao yote, sababu kubwa ya kutoweza kupata mavuno ni kwasababau hawakuwa na elimu juu ya kilimo bora.Bw. Elia anaelezea, “Hatukujua umuhimu wa kupanda kwa nafasi, kuchagua mbegu bora za maharage, kuandaa shamba kwa muda na matumizi ya mbolea na viuatilifu.”

Pamoja na kutopata mavono katika msimu wa kilimo ulio pita Bw. Elia na kikundi chake wameendelea kulima wakitumaini kuwa jitihada zao zitaonekana kama mfano kwa vijana wengine. anasema, “Ni vigumu sana kuwakusanya vijana kufanya shughuli za maendeleo katika kijiji hiki, vijana hawaoni kama kilimo ni biashara yenye fursa bali wanatazama kilimo kama ni kazi za wazee na watu masikini.”

Bi Saumu Issa ni mratibu katika shirika la Vision for Youth. Anapendelea kuona vijana wengine wakitazama kilimo kama biashara nzuri kwani rasilimali zote zinazohitajika ili kuweza kuanzisha kilimo zinapatikana kiurahisi kabisa katika mazingira yetu, na siku zote kunauhitaji wa chakula.

Shirika la Vision for Youth linawajengea uwezo vijana kwa kuwapatia mafunzo kama uandishi na utambulishi wa mipango kazi, kuandika maombi ya kibiashara na kutoa mikopo kwa biashara nzuri zilizobuniwa na vijana. Bi.Issa anasema, “Kwa ujumla aina za biashara nyingi wanazo buni vijana ni kutengeneza sabuni,shanga,bangili na viatu.” Anasema ni vigumu kuona kijana akiwa na shauku ya kufanya kilimo kama biashara, anasema, nilifurahishwa kuona Joram anapendelea kilimo.”

Bwana. Elia na wenzake wamepata mafunzo kutoka shirika la Anginet Seed Company, kama jitihada za kuhakikisha kuwa mavuno yao yanakuwa mazuri kwa msimu ujao. Sasa anapanda maharage yake kwa nafasi, sentimita 40 mstari na mstari na sentimita 20 kutoka shimo hadi shimo. Anatumia mbolea na anafanya palizi wiki moja baada ya kupanda maharage na wiki tatu baada ya palizi la kwanza. Anapanda mapema tu baada ya mvua za kwanza kunyesha na anavuna baada tu maharage yanapobadilisha rangi ya majani kuwa kiudongo. Anafanya kazi na Anginet Seed Company ili kupata uhakika wa mbegu bora na kampuni inahakikisha kuwa anapata masoko.

Kwa utaalamu huu alionao sasa Bw. Elia anaamini kuwa atapata mavuno mazuri msimu ujao.

Vision 4 Youth ni mdau wa Uniterra Tanzania. Uniterra Tanzania  inafanya kazi na wadau wa ndani wanaojihusisha na vijana, kilimo cha matunda  na mbogamboga pamoja na utalii ili kuwawezesha vijana na wanawake kuweza kujikomboa kiuchumi. Uniterra ilitoa gharama za simulizi hili.Joram Elia alipata mafunzo ya uandishi wa mpango kazi uliofanywa na mtumishi wa Uniterra Tanzania. Jifunze zaidi kuhusu Uniterra Tanzania katika Facebook kupitia: facebook.com/wusctanzania