Tuzo ya mawasililiano ya George Atkins

| Julai 9, 2019

Download this story

Tuzo ya Mawasiliano ya George Atkins ilianzishwa mwaka 1991 kutambua watangazaji wa redio za vijijini kwa juhudi zao bora na mchango wao katika kuongeza uhakika wa chakula na kupunguza umasikini katika nchi za kipato cha chini. Tuzo hiyo inaitwa kwa jina la George S. Atkins, Mkurugenzi Mwanzilishi wa shirika la kimataifa la redio kwa mkulima.

Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka kwa mtu ambaye anaonyesha ubora katika utayarishaji wa vipindi kwa jumla katika kukabiliana na mahitaji ya wakulima wadogo na kujitolea kwake kwa shirika la kimataifa la redio kwa mkulima.

Ili kustahili kupata sifa ya tuzo hii, mtu ni lazima awe amefanye kazi katika shirika ambalo limekuwa mbia na mdau wa utangazaji wa Redio kwa Mkulima chini ya mwaka mmoja. Ikiwa huna uhakika wa usahihi wa kituo chako, tafadhali wasiliana na radio@farmradio.org.

Ili kuomba tuzo ya Mawasiliano ya George Atkins, tuma fomu ya maombi iliyojazwa kikamilifu, pamoja na picha (inapendekezwa picha ya kazini ukiwa katika studio au ukifanya mahojiano) na nakala ya sauti ya kipindi chako kilichorekodiwa kwa anwani ya barua pepe zifuatazo. Tarehe ya mwisho wa maombi ni Julai 23, 2019.

Mshindi wa Tuzo ya Mawasiliano ya George Atkins atapata dola za Kanada $500 CAD na kupewa cheti katika sherehe maalum.

Tafadhali tuma maombi yako kwenye anwani mojawapo ya barua pepe zifuatazo, kulingana na unapoishi:

Burkina Faso: burkinafaso@farmradio.org
Ethiopia: ethiopia@farmradio.org
Ghana: ghana@farmradio.org
Malawi: georgevilili@gmail.com
Mali: mali@farmradio.org
Senegal: senegal@farmradio.org
Tanzania: tanzania@farmradio.org

Ikiwa unaishi katika nchi nyingine isipokuwa zile zilizoorodheshwa hapo juu, tafadhali tuma fomu yako ya maombi kwa: radio@farmradio.org

Tafadhali andika “Tuzo ya Mawasiliano ya George Atkins” kwenye kichwa cha somo katika barua pepe yako.

Pakua fomu: https://wire.farmradio.fm/wp-content/uploads/2019/07/Fomu_ya_maombi_George_Atkins_SW.doc