Method Charles | Juni 19, 2017
Rangi ya kijani katika nyumba ya Gladness Pallangyo huwa haiishi iwe ya kiangazi au masika na hii ni kwa sababu ya miti na migomba ambayo imependwa na Mama huyu katika eneo la nyumba yake ambayo pia kwa sababu ya uzuri wake na kuwa kivutio baadhi ya Watalii kutoka ndani na nje ya nchi wamekuwa wakitembelea eneo hilo. Mama Gladness anaishi mkoani Arusha wilaya ya Meru Tengeru, Patandi Kasikazini mwa Tanzania.
Licha ya serikali kuweka nguvu kidogo katika upandaji miti ili kutunza mazingira kumekuwepo wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakiunga mkono kampeni za upandaji miti ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali.
Moja ya wadau ambao wamekuwa wakipambana kwa kuotesha miche na kupanda miti ni shirika lisilo la kiserikali la Tengeru Cultural Tourism Programme lililopo Arusha kupitia mkurugenzi wake Mama Gladness ambaye amenza kazi hii tangu 1998 na mpaka sasa anamiaka 19 akifanya kazi hiyo ya uoteshaji miche na upandaji miti.
Mpaka sasa Mama Gladness amepanda 70,000 katika maeneo mbalimbali ambayo amekuwa akipanda miti.
Kutegeneza athari kubwa, jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya ni pamoja na kutembelea shule zote za msingi na shule kumi na moja za sekondari zilizopo wilayani Meru. Alisema: “Nimeomba kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wilaya cha kutembelea shule mbambali ili kuhamasisha shule zote juu ya umuhimu wa upandaji miti na kutoa mche mmoja kwa kila mwanafunzi ili aulinde na kuumwagilizia. ”
Katika safu za Mlima Meru wananchi wamekata mkaa na kuhalibu uoto wa asili na kufanya kutoweka, hali hiyo imemfanya Mama Gladness kuanza kuotesha miti katika maeneo ambayo yanaendana na Mazingira ya mlima Meru huku baadhi ya Miti ikianza kumea.
Mama Gladness kwa sasa anaendelea kuotesha miche kwa kuokota mbegu mbalimbali za miti katika maeneo ya porini na kwa kununu mbegu kwa minajili ya kuziotesha.
Mtaalamu wa masula ya hali ya hewa mkoani Dodoma Leoni Mbui amesema upandaji miti hutunza mazingira na kuwa njia moja wapo ya kutengenezwa kwa mvua hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kubuni njia mbalimbali za upandaji miti ili kuepuka kuchelewa kwa mvua kunyesha.
Mama Gladness anatumia njia za upandaji miti kwa mashindano kwa shule. Katika mashindano ya upandaji miti kwa shule mbalimbali zikiwemo shule za msingi na Sekondari shule zimekuwa na muitikio na katika mashindano ya awali shule ya Msingi Laki tatu iliyopo wilayani Arumeru ilishinda kati ya shule ishirini na moja zilizopo wilayani Meru.
Juma Msengi ni Mkuu wa Shule Laki tatu ambaye amesema miti ambayo wamepanda kwa wingi katika eno la shule imeendelea kukua na sasa wanapanda miche ya Miti na kuendelea kuhamasisha wanafunzi kuhusu umuhimu wa miti na kuwapa miche kwenda kupanda majumbani na eneo la shule.
Alisema: “Tumekuwa tukitunza miti ambayo ilitufanya tushinde katika mashindano ya shule mbalimbli kiwilaya katika zoezi la upandaji miti lililoanzishwa na Mama Gladness pia miti hii imekua na kuwa mikubwa tunaendelea kupanda michi ya miti mingine na tunahamasisha wanafunzi kutunza miti na tunazalisha miche na kuwapa wanafunzi wakaoteshe katika maeneo ya nyumbani kwao.”
Shule zingine zilizo fanya vizuri katika mashindano ya zoezi la upandaji miti ni Shule ya Sekondari Kisimiri ambayo ilikuwa nafasi ya pili ikifuatiwa na shule ya Msingi Singisi zote zipo wilayani Meru.
Licha ya kuwa Mama Gladness pia amekuwa kikumbana na changamoto mbalimbali . Alisema: amekuwa akipata changamoto mbalimbali katika katika upandaji miti kwani miche 5000 iliwahi kufa kwa kukosa maji baada ya jitihada zake binafsi kugonga mwamba kwani alikuwa peke yake na alikwa anatumia tololi kwaajili kuchota maji ya kumwagilia miche lakini alichoka.
Hata hivyo baada ya kupata changamoto hiyo aliamua kuchimba kisima cha Maji kwa mkono akishirikiana na watoto wake na alifanikiwa kupata maji na baada ya kufanikiwa kupata maji katika eneo hilo aliomba kamuni ya kuchimba kisima ikamchimbia na hivi sasa anakisima.
Na pia, baadhi ya viongozi kutuma watu kungoa miti aliyo ipanda kwa minajili ya kuwa anafanya kazi hiyo ili apate uongozi serikalini kumbe sivyo ndivyo.
Mama Gladness, alisema: “Wakati napanda miti katika maeneo ya wazi viongozi ngazi ya mtaa walingoa miti wakizani kwamba mimi napanda miti ili nikija kugombea nipite bila kupingwa kwa sababu ya kutunza mazingira.”
Lakini, anataka serikali kumsaidia kupanda miti. Mama Gladness ameomba serikali kuhamasisha kaya kuwa na eneo ambalo litapandwa miti ili kuondokana na hali ya ukame ambayo imelikumba taifa na duniani kwa ujumla.
Cultral tourism enterprises like the Tengeru Cultural Tourism Program receive support from the Tanzania Tourist Board, a Uniterra Tanzania partner. Uniterra Tanzania works with local partners in the fruit and vegetable and tourism sub-sectors to help young people and women access better economic opportunities. Uniterra provided funding for this story. Learn more and follow Uniterra Tanzania on Facebook at: facebook.com/wusctanzania