Tanzania: Wakulima wazalishaji kwa njia ya asili waona uhitaji mkubwa wa mazao yao katika masoko- ya ndani na ya nje

| Juni 19, 2017

Download this story

Mwanamseka ni kijiji kilichopo Wilaya ya  Kisarawe Mkoa wa Pwani, Kilometa  100 Magharibi mwa Mkoa wa Dar es Salaam. Udongo wa hapa ni wa kifinyanzi na hali ya hewa ni ya unyevu unyevu, ardhi ya maeneo haya ni nzuri, udongo wa kifinyanzi unakiasi kikubwa cha samadi.

Hapa ndipo Lydia Jacob na wanachama wa kikundi cha Upendo wanapanda mboga kwa njia za asili – hawatumii mbolea za viwandani wala viuatilifu vya viwandani.

Mrs. Jacob ni mama wa watoto wanne na ni mwenyekiti wa kikundi, chenye jumla ya wajumbe  16. Kwa mara ya kwanza kikundi kilianzisha kwa malengo ya kufanya ujasiria mali na biashara lakini mnamo mwaka 2014 kikundi kilielekeza malengo yake katika kilimo na kununua Ekari 22 za shamba eneo la Mwanamseka na shamba lingine kijiji cha Mafizi.

Tangu kipindi hicho kikundi cha watu 10 wamekuwa wakilima, kupanda matunda na mbogamboga kuanzia mwezi wa sita hadi mwezi wa tatu, mboga walizokuwa wakizipanda ni pamoja na okra, nyanya, tikiti maji, Chinese cabbage, spinach, vitunguu, majani ya viazi vitamu, na nyanya na wanaotesha mboga hizi kwa kutumia njia za asili.

Kilimo cha asili ni kilimo kisicho tumia kemikali, kinategemea sana sana katika mbinu za kilimo na matumizi ya mbolea na viuatilifu vya asili ili kutunza mazingira, udongo,na afya za walaji. Mboga za majani zina soko zuri ndani ya nchi na nje ya nchi ingawa bado wakulima wanajitahidi kufikia malengo ya uzalishaji, uzalishaji bado haukithi mahitaji.

Kikundi cha Upendo kinauza kwa watu na makampuni yenye uhitaji wa mboga zilizozalishwa kwa njia ya asili pamoja na masoko ya Ilala na Kariaboo Dar es Salaam. Wanatumia gari dogo la mizigo kusafirisha mboga sokoni na wakati wa mvua wanatumia pikipiki.

Bwana. Jacob anasema: “Kwa masoko ya kimataifa, tumepata oda mbili mpaka sasa, moja kutoka  Australia na Netherlands. Na hivi karibuni tumepokea oda moja kutoka Wingereza.”  

Bahati mbaya hawakuweza kutoa oda hizi kubwa za kimataifa. Bwana  Jacob anaelezea: “Tumeshindwa kutoa hizi oda kwaza kabisa kwa sababu hatuna uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa kinachohitajika [kiwango] na wateje wa kimataifa. Anaongeza: “Ubora … wa tunachokizalisha ni kidogo sana.”Kwa mfano, mteja mmoja alitaka makontena 5 hadi 6  yenye ukubwa wa futi 40 za mboga lisafirishwe kupitia bandari ya Dar es Salam, ambapo ni kiwango kikubwa sana kwa wazalishaji wadogo kama sisi.

Changamoto ya pili  ya oda za kimataifa ni upakiaji wa bidhaa,. Bwana Jacob anasema ni bei ghali kununua vifaa vya kufungia mboga ambavyo viwango vya kimataifa wanavihitaji, kwa tani moja ya mboga vifaa vya kufungashia vinagharimu karibia dola 7,000 za kimarekani sawa na shillingi milioni 15.

Anasema, ”Sisi ni wakulima wadogo hatuwezi kutoa hizi oda [wateja wa kimataifa] endapo tu tutawezeshwa. Hivi ndivyo vikwazo ambavyo vinatufanya tushindwe kufanya biashara na masoko ambayo yako tayari.”

Anatory Gabriel ni Meneja katika kitengo cha Taarifa na mawasiliano katika shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Organic Agriculture Movement, inajulikana kama  TOAM, shirika lina himiza kilimo cha  njia za asili kwa kufanya kazi na wakulima wadogo wadogo na washika dau wengine katika mnyororo wa uzalishaji.

Anasema, mazao yanayozalishwa kiasili yanasoko zuri– hapa nchini na nchi za nje. TOAM imesaidia kuwaunganisha  kikundi cha Upendo na mnunuzi kutoka  Dar es Salaam ambaye anataka kununua mboga kwa kiwango kikubwa. Ingawa anaongeza kwa kusema, “ hawa wakulima wadogowadogo hawana uwezo wa kuzalisha kukithi masoko ya ndani na hata masoko ya nje.”

Bwana Jacob anasema nguvu yao wanaipata kwa kuwa wana ardhi yenye rutuba nzuri, nzuri kwa kuotesha mazao bila kuhitaji mbolea za viwandani na madawa. Lakini wanahitaji muwekezaji kuweza kuwasaidia kifedha na utaalamu ili waweze kuboresha uzalishaji na na kununua vibebea tayari kwa kusafirisha mboga masoko ya nje.  

Kikundi cha Upendo kilivutiwa na kujihusisha na kilimo cha asili baada ya kuona matatizo ya kemikali walipokuwa wakijiusisha na uzalishaji batiki. Bwa. Jacob alisema tuliogopeshwa na kemikali baada ya kusikia kwa mwanafunzi kuwa kemikali zina madhara ya kiafya.  

Anaongeza: “Kabla hatuja jikita katika kilimo cha uzalishaji wa asili tulipata mafunzo juu ya manufaa ya kilimo cha asili ukilinganisha na madhara yanaotokana na kilimo cha kutumia kemikali.”

TOAM inatoa mafunzo haya kwa wakulima waliopo katika maeneo ya mradi. Bwana Gabriel anasema: “Kilimo cha asili kinajumuisha mbinu za asili na za kisasa, ubunifu, na sayansi ili kuweza kunufaika na mazingira yanayotumiwa kwa kilimo na mahitaji mengine na kusisitiza mahusiano mazuri na afya kwa watu wote wanaoishi kwa kutegemea mazingira.”

TOAM inawafundisha wakulima wasio weza kununua mbolea za viwandani jinsi ya kutengeneza mbolea za asili majumbani kwao kwa kutumia vitu vinavyopatikana katika mazingira. Badala ya kutumia mbolea za asili TOAM  inawahimiza wakulima kulima kilimo mseto, kutunza mabaki ya mazao baada ya kuvuna na kutokukata miti. Wanawashauri pia wakulima kutumia mbolea za asili kama mashamba yao yamepoteza rutuba.

Bwana Gabriel anasema pia tunahakikisha wakulima wanapata uelewa juu ya mabadiliko ya nchi na ukame. Anasema, “Tuna wasaidia kuelewa mazingira. Tunawafundisha mbinu mbadala za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya nchi.” Wanawashauri wakulima kupanda mazao yenye ustahimili wa magonjwa na ukame.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa mazao yanayozalishwa kwa njia ya asili, kikundi cha Upendo kinatengeneza kipato kikubwa. Nassoro Ulembo ni Baba wa watoto 5. Baba huyu wa miaka 41-anasema,  “Kilimo cha asili kimeniwezesha mimi kujenga nyumba nzuri na kulipa ada za watoto.”
 
Hamis Makunganya ni mwanachama mwingine wa Upendo group. Baba huyu wa Miaka 43 na watoto 5-anaishi kijiji cha  Mafizi, Anasema, “Kupitia kilimo cha asili nimeweza kujenga nyumba mbili na nimetumia hela nyingine kulipa ada za watoto wangu.”
 
Tanzania Organic Agriculture Movement ni sehemu ya mradi wa Uniterra Tanzania. Uniterra Tanzania inafanya kazi na washikadau katika kilimo cha matunda na mboga mboga pamoja na utalii -inasaidia vijana na wanawake  kuoata uchumi bora. Uniterra imegharamia gharama za kuandika simulizi hili. Kwa maelezo na kujifunza zaidi penda Uniterra Tanzania katika  Facebook kupitia : facebook.com/wusctanzania