Tanzania: Wanafunzi wanapanda miti zaidi kuepusha jangwa

June 19, 2017
A translation for this article is available in French English

Rangi ya kijani katika nyumba ya Gladness Pallangyo huwa haiishi iwe ya kiangazi au masika na hii ni kwa sababu ya miti na migomba ambayo imependwa na Mama huyu katika eneo la nyumba yake ambayo pia kwa sababu ya uzuri wake na kuwa kivutio baadhi ya Watalii kutoka ndani na nje ya nchi wamekuwa wakitembelea eneo hilo. Mama Gladness anaishi mkoani Arusha wilaya ya Meru Tengeru, Patandi Kasikazini mwa Tanzania.

Licha ya serikali kuweka nguvu kidogo katika  upandaji miti  ili kutunza mazingira kumekuwepo wadau  mbalimbali  ambao wamekuwa  wakiunga mkono  kampeni za upandaji miti  ambazo  zimekuwa zikifanywa na serikali.

Moja ya wadau ambao wamekuwa wakipambana  kwa kuotesha  miche  na kupanda  miti  ni shirika lisilo la kiserikali  la Tengeru Cultural Tourism Programme lililopo Arusha kupitia mkurugenzi wake  Mama Gladness ambaye  amenza kazi  hii  tangu 1998  na mpaka sasa  anamiaka 19 akifanya kazi hiyo ya uoteshaji  miche na upandaji miti.

 Mpaka sasa Mama Gladness  amepanda  70,000 katika  maeneo mbalimbali  ambayo amekuwa akipanda miti.

Kutegeneza athari kubwa,  jitihada ambazo  wamekuwa  wakizifanya ni pamoja  na   kutembelea shule zote za msingi  na  shule kumi na moja  za  sekondari  zilizopo wilayani  Meru. Alisema: “Nimeomba kibali kutoka  kwa Mkurugenzi  wa wilaya cha kutembelea shule mbambali ili kuhamasisha  shule zote  juu ya umuhimu wa upandaji miti  na kutoa mche mmoja  kwa kila mwanafunzi ili aulinde na  kuumwagilizia. ”

Katika safu za Mlima Meru wananchi wamekata mkaa na kuhalibu uoto wa asili na kufanya kutoweka, hali hiyo imemfanya Mama Gladness kuanza kuotesha miti katika maeneo ambayo yanaendana na Mazingira ya mlima Meru huku baadhi ya Miti ikianza kumea.
Mama Gladness kwa sasa anaendelea  kuotesha miche  kwa kuokota mbegu mbalimbali  za miti katika maeneo  ya porini  na kwa kununu mbegu kwa minajili ya kuziotesha.

Mtaalamu wa masula ya hali ya hewa   mkoani Dodoma  Leoni Mbui amesema upandaji miti hutunza mazingira  na kuwa njia moja wapo ya kutengenezwa kwa mvua hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kubuni njia mbalimbali za upandaji miti ili kuepuka kuchelewa kwa mvua kunyesha.

Mama Gladness anatumia njia za upandaji miti kwa mashindano kwa shule. Katika mashindano  ya upandaji  miti kwa shule mbalimbali zikiwemo  shule za msingi na Sekondari  shule zimekuwa na muitikio   na katika mashindano ya awali shule ya Msingi Laki tatu  iliyopo wilayani Arumeru  ilishinda kati ya shule ishirini na moja  zilizopo wilayani Meru.
Juma Msengi  ni Mkuu wa Shule Laki tatu ambaye  amesema miti ambayo  wamepanda  kwa wingi katika  eno la shule imeendelea kukua  na sasa wanapanda miche ya Miti  na kuendelea  kuhamasisha  wanafunzi  kuhusu umuhimu wa miti  na kuwapa miche kwenda kupanda majumbani na  eneo la shule.

Alisema: “Tumekuwa tukitunza miti ambayo ilitufanya tushinde katika mashindano ya shule  mbalimbli kiwilaya katika zoezi la upandaji miti lililoanzishwa na Mama Gladness pia miti hii imekua  na kuwa mikubwa  tunaendelea kupanda michi ya miti mingine  na tunahamasisha wanafunzi kutunza miti na tunazalisha  miche  na kuwapa wanafunzi wakaoteshe katika maeneo ya nyumbani kwao.”

Shule zingine zilizo fanya vizuri katika  mashindano ya  zoezi la upandaji miti  ni  Shule ya Sekondari Kisimiri  ambayo ilikuwa nafasi ya pili ikifuatiwa na  shule ya Msingi  Singisi  zote zipo wilayani Meru.

Licha ya kuwa Mama Gladness  pia amekuwa kikumbana na changamoto mbalimbali . Alisema: amekuwa akipata changamoto mbalimbali katika  katika  upandaji miti  kwani miche 5000 iliwahi kufa kwa  kukosa maji  baada ya jitihada zake binafsi kugonga mwamba  kwani alikuwa peke yake  na alikwa anatumia tololi kwaajili kuchota maji ya kumwagilia miche  lakini alichoka.

Hata hivyo baada ya kupata changamoto hiyo  aliamua  kuchimba kisima cha Maji  kwa mkono akishirikiana na watoto wake na alifanikiwa kupata maji  na  baada ya  kufanikiwa kupata maji katika eneo hilo  aliomba kamuni ya kuchimba kisima ikamchimbia na hivi sasa anakisima.  

Na pia, baadhi ya  viongozi  kutuma watu kungoa miti  aliyo ipanda  kwa minajili ya kuwa  anafanya kazi hiyo ili  apate uongozi serikalini  kumbe sivyo ndivyo.

Mama Gladness, alisema: “Wakati napanda miti  katika maeneo  ya wazi viongozi ngazi ya mtaa walingoa miti wakizani kwamba mimi napanda miti ili nikija kugombea nipite  bila kupingwa  kwa sababu  ya kutunza mazingira.”

Lakini, anataka serikali kumsaidia kupanda miti. Mama Gladness ameomba  serikali  kuhamasisha  kaya kuwa na eneo  ambalo litapandwa miti ili kuondokana na hali ya ukame ambayo  imelikumba taifa na duniani kwa ujumla.

Cultral tourism enterprises like the Tengeru Cultural Tourism Program receive support from the Tanzania Tourist Board, a Uniterra Tanzania partner. Uniterra Tanzania works with local partners in the fruit and vegetable and tourism sub-sectors to help young people and women access better economic opportunities. Uniterra provided funding for this story. Learn more and follow Uniterra Tanzania on Facebook at: facebook.com/wusctanzania