Joseph Tsongo | Juni 10, 2020
News Brief
Kabla ya kuanza kwa janga la COVID-19 na marufuku ya matumizi ya nyama pori, sheria za Kongo zilikuwa zimepiga marufuku ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa kama Hifadhi ya Taifa ya Virunga, iliyoainishwa kama Eneo la Urithi wa Dunia. Lakini wawindaji kama Bwana Kaposolina waliendelea kuingia na kuwinda kama wawindaji haramu. Bwana Kaposolina anasema: "Ninaishi hapa. Kila siku, lazima niamke kabla ya saa tano asubuhi ili kuangalia mitego yangu msituni na kukusanya mawindo yangu ... lakini leo siendi huko na wateja wangu wanateseka kama mimi." Kabla ya kuanza kwa janga la COVID-19 na marufuku ya matumizi ya nyama pori, sheria za Kongo zilikuwa zimepiga marufuku ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa kama Hifadhi ya Taifa ya Virunga, iliyoainishwa kama Eneo la Urithi wa Dunia. Lakini wawindaji kama Bwana Kaposolina waliendelea kuingia na kuwinda kama wawindaji haramu.
Ni saa moja asubuhi na mvua nzuri inanyesha katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga huko Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Paluku Kaposolina, ambaye anaishi katika eneo hilo, anainama ili kuwasha moto karibu na kibanda chake. Bwana Kaposolina ana miaka 30 tu, muonekano wake humfanya aonekane ni mzee.
Kijana huyu hutegemea uwindaji haramu kwa ajili ya kujipatia chakula. Hatahivyo, kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa virusi kama vile Ebola na ugonjwa wa virusi vipya vya Corona, ambayo magonjwa yote haya yalitoka kwa wanyama, uwindaji na utumiaji wa nyama pori umepigwa marufuku rasmi. Kuna kampeni za uhamasishaji kuhakikisha kila mtu anaelewa ujumbe huu. Lakini jamii zinazoishi karibu na misitu zinapata shida kufuata marufuku hii kwa sababu zimekuwa zikipata protini yao nyingi kutoka kwa nyama pori kwa kipindi cha muda mrefu.
Bwana Kaposolina anasema: “Ninaishi hapa. Kila siku, lazima niamke kabla ya saa tano asubuhi ili kuangalia mitego yangu msituni na kukusanya mawindo yangu … lakini leo siendi huko na wateja wangu wanateseka kama mimi.”
Kabla ya kuanza kwa janga la COVID-19 na marufuku ya matumizi ya nyama pori, sheria za Kongo zilikuwa zimepiga marufuku ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa kama Hifadhi ya Taifa ya Virunga, iliyoainishwa kama Eneo la Urithi wa Dunia. Lakini wawindaji kama Bwana Kaposolina waliendelea kuingia na kuwinda kama wawindaji haramu.
Malese Yirayira ni kiongozi wa jamii na mtaalam wa magonjwa ya mifugo, na ana wasiwasi kuwa mlo na mila za jamii zitatatizwa na marufuku ya uwindaji. Anaelezea, “Ikiwa marufuku ya uwindaji au matumizi ya wanyamapori itaendelea, mamilioni ya watu katika jamii za asilia au vijijini ambao hutegemea moja kwa moja nyama pori kwa protini watakuwa kwenye hatari ya utapiamlo.”
Anasema kwamba vikundi vingi katika mkoa huu huishi kwa kuwinda wanyama wa porini kama nyani, mbweha, njiwa za mwituni, ngiri, panya, swala, nyati, na wanyama wengine wengi. Vikundi vingine pia hutumia wanyama hawa kama dhabihu za kimila kuwasiliana na mababu na kutatua shida za jamii.
Kuambukizwa kwa magonjwa kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu sio jambo jipya. Kulingana na Vituo vya Amerika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, tatu kati ya kila magonjwa manne mapya au yanayojitokeza kwa watu hutoka kwa wanyama. Nakala hiyo inaonyesha kwamba wakati magonjwa yanaambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu, inaweza kuwa mbaya zaidi na inaweza kusababisha majanga wakati yanaenea kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
Bahati Kiro ni mtaalam wa magonjwa ya wanyama. Bwana Kiro anafafanua: “Magonjwa yatokanayo na wanyama ni magonjwa ya kuambukiza ambayo huwafikia wanadamu kupitia wanyama. … Ni katika muktadha huu kwamba kula nyama pori ni marufuku leo hata hapa nchini DRC. Ni wazi kwamba shinikizo la wanadamu kwa viumbe hai husababisha shida.”
Katika eneo hili, idadi kubwa ya watu wanakiuka sheria za maeneo yaliyohifadhiwa kama Hifadhi ya Taifa ya Virunga kwa kukata miti au kulima ardhi, lakini pia kuwinda wanyama wa porini. Mkaa ni tasnia yenye kustawi na hakuna ardhi ya kutosha ya kilimo katika mkoa huo, na wanyama hutumiwa kwa chakula na biashara. Shughuli hizi zinafanywa na kupata baraka kutoka kwa vikosi vyenye silaha vilivyo na nguvu katika mkoa huo.
Ingawa asili ya janga la virusi vya Corona na njia halisi ya maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu bado haijafafanuliwa, kuna ufahamu kwamba virusi vilienea kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu.
Lakini nyama-na hasa nyama ya mwituni – sio njia pekee ya kupata protini. Bantu Lukambo ndiye mratibu wa shirika la eneo hili linalolinda mazingira na kuchochea maendeleo endelevu mashariki mwa DRC. Anaelezea kuwa mahitaji ya protini ya kila mtu ni tofauti na imedhamiriwa na sababu nyingi, pamoja na uzani wa mwili. Anasema, “Tunaweza kupata protini kutoka kwa mimea kama tuwezavyo kutoka kwa wanyama. Mwili wa mwanadamu unahitaji proteni za aina zote.”
Shirika lake tayari limeanzisha kibanda cha jamii kwa ajili ya kufuga wanyama wadogo na shamba la uyoga kusaidia wakulima kukuza uyoga karibu na Hifadhi Taifa ya Virunga katika juhudi za kupunguza ujangili na utumiaji wa nyama pori.
Rasilimali hii imeandaliwa kwa msaada wa kifedha kutoka kwa serikali ya Canada uliotolewa kupitia Global Affairs Canada.