- Barza Wire - https://wire.farmradio.fm -

Tuzo ya Liz Hughes kwa vituo vya redio vyenye kuhamasisha masuala ya usawa wa kijinsia

Farm Radio International imeandaa tuzo mpya zinazotambua vituo vya redio vinavyohamasisha na kutoa vipindi vinavyozungumzia masuala ya kijinsi na kupaza sauti za wanawake wa vijijini. Farm Radio International inaalika vituo vya redio na timu ya uzalishaji vipindi kutuma maombi yao kwaajili ya kushiriki katika tuzo hii ya Liz Hughes.

Liz Hughes alikuwa ni mjumbe wa bodi wa Shirika la Farm Radio na alikuwa na shauku kubwa katika utangazaji na pia alikuwa ni bingwa katika masuala ya jinsia. Shirika la Utangazaji la Kanada lilisaidia shirika la Farm Radio kuandaa mfumo uitwao FAIR journalistic standards [1], mfumo huu unahimiza usawa na haki, uadilifu na heshima kwa watu wote.

Vijiji barani Afrika, nchi za kusini mwa jangwa la sahara, wanawake wanamchango mkubwa katika shughuli za kilimo na jamii kwa ujumla. Lakini wanahatari kubwa ya kukumbwa na janga la njaa, utapiamlo, na udhaifu wa afya, na hawana haki ya kumiliki au utumiaji wa mali au rasilimali. Ni muhimu kituo cha redio kuhimiza mahitaji na vipaumbele vya wanawake na wanaume pia. Ili wote wanaume na wanawake waweze kunufaika na taarifa zinazotolewa na kuweza kuchangia katika maendeleo ya jamii. Jifunze zaidi jinsi ya kuweza kuwahudumia wanawake wakulima katika chanzo hiki cha taarifa kwa watangazaji [2].

Kituo chochote cha redio barani Afrika kinaweza kutuma maombi yake kushindania tuzo hii. Wanapaswa kutuma kipindi chochote cha redio ambacho wanaona kuwa kilihimiza masuala ya kijinsia. Kituo kimoja cha redio kinaweza kutuma maombi mbali mbali kama kina vipindi mbalimbali vyenye vigezo vilivyotajwa.

Watuma maombi wanalazimika kujaza fomu ya maombi na kuambatanisha rekodi kwa mfumo wa MP3, fomu na rekodi zote zitumwe kwenda radio@farmradio.org. Tafadhali kichwa cha habari kiwe: Liz Hughes Award for Her Farm Radio

Maombi yatapokelewa katika lugha ya kingereza, French, Amharic, Swahili, na Hausa. Rekodi utakayoambatanisha inaweza kuwa imerekodiwa kwa lugha ya mahali husika.

Mwisho wa kutuma maombi ni mwezi wa kwanza, tarehe 17, 2020.

Timu au kituo cha redio kitakachoshinda tuzo hii kitapokea cheti na kiasi cha dola za Kikanda 1,000 kama kutambua ubora wa kazi yao.

Pakua fomu ya maombi hapa: https://wire.farmradio.fm/wp-content/uploads/2019/12/Liz-Hughes-Award-Application-form-2020-SW.docx