Jiunge na kampeni yetu ya kuamini chanjo

| Machi 18, 2022

Download this story

Chanjo ni muhimu katika kuzuia kuumwa sana kama matokeo ya COVID-19 na kuweka jamii zetu zikiwa na afya. Watu wengi bado wana maswali au wanasitasita kuhusu chanjo za COVID-19. Kama mtangazaji, wewe ni sauti inayoaminika na inayoheshimiwa katika jamii yako. Unawafikia maelfu ya wanaume, wanawake, wavulana na wasichana kupitia programu yako. Paza sauti yako kwasababu ni muhimu! Jiunge na kampeni yetu ya kutangaza chanjo za COVID-19, jibu maswali ya wasikilizaji wako, na utoe maelezo mazuri kuhusu upatikanaji na ufanisi wa chanjo zinazopatikana katika jamiiyako.

Farm Radio International inashirikisha washirika wa redio katika nchi 16 katika kampeni yetu ya kuamini chanjo, ambayo itakuwa hewani kati ya mwezi Mei na Agosti 2022. Tungependa ujiunge nasi kutangaza habari njema kuhusu COVID-19 kwenye redio yako. 

Tutaunda kampeni hii pamoja, tukichagua ujumbe na mada muhimu ambazo zinaendana na hadhira yako na kushughulikia mahitaji ya habari ya wasikilizaji wako. Kampeni itajumuisha sehemu za redio na sehemu za mahojiano ambazo unaweza kurusha kwenye vipindi vingi kwenye kituo chako. Tunataka kuwafikia watu wengi iwezekanavyo na jumbe hizi: vijana kwa wazee, wanaume, wanawake, wasichana na wavulana. 

Katika kampeni hii, kituo chako kita:

  • Shughulikia habari za uwongo na habari zisizo za kweli
  • Jibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara kutoka kwa wasikilizaji wako kuhusu COVID-19 na  chanjo za COVID-19
  • Himiza chanjo dhidi ya COVID-19 katika jamii yako
  • Hakikisha wanawake na wanaume wana taarifa wanazohitaji ili kuhakikisha kuwa wako salama dhidi ya COVID-19
  • Na mengine zaidi!

Ni wakati wa kuchukua hatua kuhusu COVID-19. Jiunge na kampeni yetu. Bonyeza hapa kujisajili.

Maelezo ya kampeni

Ukikubali kujiunga na kampeni yetu, utajitolea kutangaza angalau dakika 50 za programu kila wiki kuhusu chanjo za COVID-19, hatua za kuhakikisha usalama wa Afya kwa umma (barakoa, kukaa umbali kati ya mtu na mtu, unawaji mikono, n.k), ​​na masuala yanayohusiana na usawa wa kijinsia kwa wiki 10-12. (Muda kamili wa kampeni utabainishwa kupitia majadiliano na mamlaka za Afya za eneo lako ili kuongeza matokeo chanya ya kampeni hii.) Kampeni hii itajumuisha sehemu za mahojiano zitakazorushwa kwa angalau vipindi 5 tofauti katika kituo chako. Hii inaweza kujumuisha kipindi chako cha michezo, muziki, siasa, au programu za vijana, pamoja na programu za wakulima, programu za Afya na programu nyinginezo. Kampeni hiyo pia itajumuisha matangazo ya redio, jingo, matangazo ya utumishi wa umma na miundo mingine. 

Pia tunatumai kuwa utashirikisha ujumbe wa kampeni hii kwenye chaneli zako za mitandao ya kijamii.

Utakuwa na fursa ya kuunda kampeni hii kwa kushiriki katika mchakato wa kuunda programu hii pamoja na Farm Radio, redio nyingine katika nchi yako, na wadau husika, ikiwa ni pamoja na mashirika ya Afya, mashirika ya kijamii, na vikundi vya wanawake. 

Pia tutakuomba utangaze matangazo yanayotangaza kura yetu ya Uliza, ambayo ni jukwaa la kukusanya maoni kutoka kwa wasikilizaji wako. Maoni haya yatatusaidia kujifunza zaidi kuhusu mahitaji ya taarifa ya hadhira yako na matokeo ya kampeni.

Kama sehemu ya kampeni, tutatoa vipindi vya mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ujuzi wa redio na miundo, ikijumuisha matumizi ya matangazo ya redio. Vipindi hivi vya mafunzo vitatumia moduli zetu za kujifunza mtandaoni ambazo ni kikundi cha WhatsApp na Zoom. Vipindi hivi vya mafunzo pia vitatoa fursa ya kukutana na wataalamu wa somo husika na kukusanya taarifa zinazohitajika ili kuunda ujumbe wa kampeni. Mwishoni mwa kipindi cha wiki tatu, timu yako itakuwa imechangia katika kuunda muundo wa kampeni. Mafunzo na kuunda muundo huu itaanza Aprili.

Farm Radio pia itakuwa ikitayarisha miongozo mingi ya redio, matangazo, simulizi na rasilimali nyinginezo ili kufahamisha kampeni.

Utaombwa kuonyesha ushiriki wako kwa kushirikisha rekodi zilizochaguliwa za matangazo na vipengele utakavyorusha hewani. Utapewa uwezo wa kuingia kwenye jukwaa letu la Uliza ili kuweka rekodi zako. Utahitaji pia kuwasilisha ripoti inayoelezea tarehe na muda ambao ulitangaza matangazo na sehemu zote za kampeni.

Farm Radio International itakuwepo kukusaidia katika kila hatua. Maafisa wetu wa mitandao watakuwepo wakati wote wa mafunzo na unapokuwa hewani ili kukusaidia kupata rasilimali na kuwahoji wageni, na kujibu maswali yoyote.
Tunayo furaha kutoa heshima ndogo kwa vituo vyote vya redio vinavyoshiriki kikamilifu katika kampeni. Tutakuandikia na kukutumia barua ya heshima ya kutambua mchango wako ikiwa utaonyesha nia yako ya kushiriki katika kampeni. Jisajili hapa: https://forms.gle/MJXVXqiqkxRuYu796