- Barza Wire - https://wire.farmradio.fm -

Tanzania: Wakulima watunza udongo kwa kufanya kilimo hifadhi, kukwatua kwa kina kifupi na kuacha mabaki ya mazao shambani

Cette nouvelle a été publiée en juin 2018. / This story was originally published in June 2018

Anga jeupe na jua likiwaka katika milima kijani yenye miinuko mikali katika maeneo ya mlima Meru kaskazini mwa Tanzania. Mkulima Bi. Felix Nassari akiangalia kama mabua ya mahindi ya msimu uliopita kama yameoza vizuri shambani ili ajiandae kupanda karoti kwa msimu huu. Anasema, “Kabla sijapanda ninaacha mabaki ya mazao ya msimu uliopita yaoze shambani.”

Mama wa-miaka-32 na binti yake wa-miaka-sita wanaishi kijiji cha Ndoombo katika njanda za juu za Meru, kama kilomita 40 kutoka mji wa Arusha. Katika eneo hili wakulima wengi wanalima kilimo hifadhi ili kukabiliana na mmomonyoko wa udongo kama anavyofanya Bi. Nassari. Hii inawawezesha wakulima wanaoishi katika maeneo haya yenye mteremko mkali na yanayokumbwa na mmomonyoko wa udongo kutokana na mafuriko yatokayo milimani kuweza kulima.

Bi. Nassari analima na kubadilisha mahindi, kabichi, viazi, na karoti katika shamba lake la hekari mbili. Baada ya kuvuna mahindi anaacha mabua kuoza na kuwa mbolea shambani.

Pia anatengeneza matuta na kwa umakini anatumia jembe lake la mkono kupiga mashimo shambani. Hii unasaidia kuepuka kumomonyoka kwa udongo wa juu wenye rutuba. Anaelezea: “Ninatengeneza matuta [katika kila sentimita 70 kwenye miteremko] kupunguza kasi ya maji shambani, na nina panda kwa kutumia jembe la mkono. Nina epuka kuchimba mashimo marefu kuepuka kutengeneza mitaro ya maji.”

Sheilah Yusuf ni afisa ugani katika eneo hili. Alipoanza kufanya kazi miezi 18 iliyopita katika maeneo haya ya miteremko, alishangaa sana jinsi wakulima wanavyoweza kuzalisha katika eneo hili.

Anasema: “Kwa mara yangu ya kwanza kutembelea mashambani, nilishangazwa sana jinsi wakulima wanavyoweza kuzalisha katika maeneo haya ya miinuko mikali ya miteremko. Kwa miaka mingi wamejifunza wenyewe jinsi ya kutunza ardhi yao.”

Bi. Yusuf anasema, katika maeneo ya miteremko mikali ya meru wakulima wamekuwawakilima kiliomo hifadhi kwa miaka mingi kukabiliana na mmomonyoko wa udongo. Mbinu hizi ni pamoja na kutengeneza matuta, kukwatua kwa kina kidogo, kilimo mseto na kilomo mzunguko, na kuacha mazao kuoza shambani baada ya mavuno.

Julius Naftari Nasari analima katika hekari tatu, anachanganya mahindi na maharage na baada ya kuvuna mahindi yake anapanda karoti na viazi.

Bw. Nasari anasema anapendelea kulima kwa jembe la mkoni ili asisumbue muundo wa udongo. Ansema kulima kwa jembe la mkono ni rahisi kuliko kulima kwa trekta kwasababu ni vigumu kupandisha trekta katika miinuko.

Anaongeza: “Mashamba yako katika miteremko mikali, wakati wa kipindi cha mvua shamba lako linabidi liwe na udongo mzuri wenye uwezo wa kukinga mmomonyoko; kinyume na hapo, rutuba yote itachukuliwa na mafuriko.”

Bw. Nasari anapalilia kwa mikono na anaongeza mboji shambani kuboresha udongo.

Lakini Bw. Nasari ansema mbinu hizi zinahitaji vibarua. Anaelezea: “Inachukua muda mrefu kupalilia kwamikono, kupanda kwa kutumia jembe la mkono, na inagharimu kuongeza mbolea juu ya majani ili kuboresha udongo. Lakini hii ni namna pekee ambayo tunaweza kulima na kuvuna katika eneo hili.”

Kulingana na Bw. Nasari, siri ya kuweza kupata mavuno mazuri katika eneo hili ni kutunza ardhi. Ansema sikuzote wanunuzi wanaokuja kununua mazao katika maeneo haya wanashangazwa sana jinsi wakulima wanavyoweza kulima vizuri katika maeneo haya ya muinuko yenye miteremko mikali. Wanunuzi wanalazimika kuacha magari yao barabarani na kubeba magunia ya mazao begani kupeleka kwenye gari kwasababu magari hayawezi kupanda milimani.

Mbali na changamoto katika miinuko hii, Bw. Nasari anasema kwa miaka mingi wakulima katika maeneo haya wameweza kuzalisha mazao mengi ambayo yanauzwa masoko ya karibu na mengine yakiuzwa mpaka Arusha mjini.

Bw. Nassari anasema, kwa kutumia mbinu kama kulima kwa kina kifupi na kiacha mabaki ya mazao kuoza shambani kumemsaidia kuboresha udongo.

Msimu uliopita Bi. Nassari alivuna gunia 40 za karoti na gunia 50 za viazi mviringo, kila guni lina ujazo wa kilo 100. Anauza karoti kwa shilingi 500-700 (sawa na dola US$0.22-0.31) kwa kilo, na na viazi kwa 800 shillingi (sawa na dola US$0.35) kwa kilo.

Anasema, kupitia kilimo, amemsaidia mume wake kujenga nyumba nzuri yenye bati. Kwa kuongezea sasa wanamaji ya uhakika nyumbani kwao.

Kazi hii imefanywa na msaada wa Canadian Foodgrains Bank kama sehemu ya mradi, “Kilimo hifadhi kujenga usatahimili, kilimo cha kisasa cha kuzingatia hali ya mazingira.” Kazi hii imefadhiliwa na serikali ya Canada, kupitia Global Affairs Canada, www.international.gc.ca.