- Barza Wire - https://wire.farmradio.fm -

Tanzania: Mbinu bora za kilimo za boresha mavuno ya viazi

Ni majira ya saa takribani saa mbili asubuhi, Bibi Everna Mfuse akivuna viazi vyake katika shamba la ekari moja na nusu akisaidiwa na marafiki zake, anaonekana akiwa amevaa gauni la rangi ya njano,nyekundu, pamoja na suruali nyeusi. Mama huyu mwenye umri wa miaka 42-anasema kuwa huu ni mwaka wa neema kwani kwa kipindi cha nyuma mavuno yalikuwa ya chini kiasi ya kwamba hakuhitajii marafiki zake wamsaidie.

Bibi. Mfuse anasema: “Nilianza kulima viazi mviringo mnamo mwaka 1994 na kipindi hiki cha nyuma siku jua umuhimu wa kuchagua mbegu bora na matumizi sahihi ya mbolea na madawa.Katika shamba la ekari moja nilikuwa nikivuna gunia tani tu za viazi.”

Bibi. Mfuse anaishi na wanawe wawili katika kijiji cha Nundu mkoani Njombe nyanda za juu kusini mwa nchi ya Tanzania. Mkoa huu huwa unapokea kiwango kikubwa cha mvua kwa kipindi cha mwaka mzima na ina udongo wenye rutuba.

Mwaka2012, Bibi. Mfuse alihudhuria maonyeshi ya wakulima wilayani Uyole mkoa wa Mbeya, ambapo aliweza kujifunza namna ya kupanda viazi kwa njia za kisasa.

Anasema mbinu zake za kulima viazi ziliaongezaeka kutokana na mafunzo anayopatiwa na maafisa ugani na mafunzo wanayopata katika kikundi.

Anasema sasa anajua namna ya kupanda viazi kwa nafasi zilizo shauriwa: sentimita 60-75 kutoka mstari hadi mstari na 20-25 sentimita kutoka shimo na shimo, kulingana na aina ya mbegu. Pia anauelewa mzuri wa mbinu za kusafisha shamba, matumizi ya mbolea na matumizi ya dawa pamoja na umwagiliaji wa shamba lake.

Anaongeza kwa kusema,: “Ninapendelea kupalilia kwa jembe la mkono na juwa ninapofanya palizi ninaacha mabaki ya majani shambani kuoza na kurutubisha ardhi. Sasa nina vuna viazi mwaka mzima; na katika shamba la ekari 1 badala ya kuvuna magunia 5, sasa ninavuma magunia 120 ya viazi.”

Chelina Mlingo ni mkulima wa viazi ambaye ananunua vipando vya viazi kutoka kwa Bibi. Mfuse. Lakini kwa siku ya leo yuko shambani kwake akimsaidia kuvuna. Lengo lake ni kuwa mkulima hodari kama Bibi. Mfuse, na anajifunza mambo mengi kutoka kwake.

Telesia Mcha ni mkurugenzi wa shirika la Stawisha, shirika linalo fanya kazi kwa ukaribu kabisa na wakulima wa viazi mviringo na kuwa himiza walime viazi bora. Bw. Mcha anaelezea kuwa, mbali na kuwapatia wakulima mafunzo na kuwapatia vipando vya viazi, shirika pia linawashawishi wafanya biashara kuwekeza katika uzalishaji wa viazi.

Anasema: “Tunataka kufanya mapinduzi ya kilimo cha viazi …kuhama kwenye kilimo cha jembe la mkono na kulima kilimo cha mashine. Wakulima wanapaswa kutumia mashine kupanda, kupalilia na kuvuna ili kuwawezesha kupata mavuni yenye tija.”

Mwaka huu, Bibi. Mfuse atapanda hekari tatu za viazi mviringo. Anategemea kuvuna kama gunia 350 na kuuza kwa kiasi cha shillingi 17,500,000 sawa na dola (7,650 za kimarekani).

Alianza kulima viazi na mtaji wa shilingi 100,000 sawa na dola (44 za kimarekani), lakini sasa anakiasi cha shilingi milioni tano (kama dola 2,200 za kimarekani), ng’ombe wanne wa kukamua, na nyumba nzuri ya matofali, na nyumba ya vyumba 12-za kupangisha.

Anaongeza: “Nina watoto wawili ambao wanasoma katika shule nzuri. Nina walipia ada na nimeweza kuongeza eneo la kulimia viazi. Pia nina uza vipando vya mbegu kwa wakulima wengine.”

Simulizi hili limeandaliwa na msaada wa USAID New Alliance ICT Extension Challenge Fund, kupitia mfuko wa msaada wa kimataifa wa kilimo Tanzania.
This story was prepared with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/ [1]