- Barza Wire - https://wire.farmradio.fm -

Tanzania: Athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mifugo na wafugaji

Akiwa ameweka mikono yake nyuma, Mhache Paulo anatazama kwa umakini uani mwa nyumba yake na mdomo wa Agape. Mr Paulo anasema kwamba miaka 15 iliyopita alikua akitazama mazingira mazuri ya kijani na mito isiyo na mwisho. Lakini leo kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, yale mazingira ya kijani yamepotea- hakuna miti na hakuna maji yanayotiririka katika mito. Anasema, “Mabadiliko ya tabia nchi yameathiri mfumo wa ikolojia.”

Bw. Paulo ni mfugaji mdogo katika jiji la Dar Es Salaam, Jiji la kibiashara Tanzania. Alianza ufugaji wa kuku mnamo mwaka 1999.
Anasema, joto kali na mabadiliko ya mara kwa mara ya hali ya hewa kama vile ukame umathiri sio tu mazingira ya nyumbani kwake bali hata shughuli zake za ufugaji. Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwepo na milipuko ya magonjwa ya mifugo, ukosefu wa malisho na uhaba wa maji.

Bw. Paulo alikua na zaidi ya nguruwe 100 mnamo mwaka 2018. Lakini kati ya mwezi wa sita na wa tisa mwaka huo, Homa ya nguruwe, ugonjwa hatari na unaoambukiza kwa kasi uliua nguruwe zake zote.

Anaeleza “Ilikua ni majanga. Ugonjwa huu haukua katika eneo hili… lakini inawezekana uliletwa na watu ambao walikua wanasafirisha mifugo kutoka vijijini kuelekea jijini.”

Maziku Methew ni Mtaalamu wa mifugo kutoka katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania, anasema mabadiliko ya tabia nchi yanafukuza ndege pamoja na wanyama wengine kutoka katika maeneo yao ya kawaida na kwenda kutafuta chakula na maji.

Methew aliongeza kua “Kitendo hiki cha wanyama kuhama kutoka eneo moja na kwenda katika eneo jingine kuna ambatana na kueneza magonjwa ambayo yanasababisha janga katika eneo hilo jipya.”

Pia, mabadiliko ya tabia nchi yameathiri bwawa la samaki la Bw. Paulo. Alisema, “Jua lililopiga jiji mwezi Julai limekausha bwawa lote. Sijui nitafanya nini kwa muda ulibaki wa mwezi hadi hapo mvua itakaponyesha.”

Alieleza kua, jua limekua likipasha maji moto na kusababisha samaki kwenda katika kina cha chini ambapo kuna oksijeni kidogo ambapo inapelekea kupata shida katika upumuaji.

Anasema kwamba pia mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri ndege zake kama aina ya kanga na kuku kwa sasa wanasumbuliwa sana na magonjwa kama ndui.
Agnes Victor ni mfugaji wa kuku kutoka Salasala katika viunga vya jiji la Dar Es Salaam. Anasema hali ya hewa kati ya mwezi wa sita hadi wa tisa ilikua kame/ kavu kuliko kawaida ambapo ilipelekea kuwepo na magonjwa yanayosababishwa na virusi kama vile ndui inayosambaa kwa kasi sana katika eneo lake, na kuua kuku na hasa wale ambao hawajapata chanjo kwa wakati.

Bi. Victor anasema “Wamekua wakilazimika kutumia fedha kwenye chanjo. Garama za kufuga kuku zinazidi kuongezeka kwa sababu ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.”

Anasema kwamba kiangazi cha muda mrefu na ongezeko la joto limepunguza sana mavuno ya mazao ambayo hutumika kama chakula cha mifugo na kusababisha kuongezeka kwa garama za malisho. “Mfuko wa chakula cha kuku inagharimu kati ya shilingi 60,000 hadi 80,000 kwa pesa ya Tanzania (ambayo ni dola 26-35 za Marekani), kutegemea na eneo.”

Bw. Paulo na wakulima wengine kama Bi. Victor wanafanya shughuli mbalimbali za kilimo ili kuongeza vyanzo vya malisho ili kuthibiti athari zilizopo.

Wafugaji wanaoishi Dar es Salaam wanasema kwamba kwa sasa wanachimba visima, na kuanzisha mifumo ya umwagiliaji ili kusaidia familia zao kupata malisho. Wameanza kujishugulisha na mazao kama vile ndizi, mihogo and maharage pamoja na kufuga ngombe.

Bi. Victor anasema “Mara nyingi kutokana na mvua kutotabirika tunapanda mazao yanayostahimili ukame au mazao yanayokomaa kwa muda mfupi.” Ameongeza kua “Kufanya kilimo mseto na kupanda miti – hasa miti ya asili kunatoa malisho bora na kivuli kwaajili ya mazao.”

Bw. Paulo alichimba kisima na kujenga bwawa kwa ajili ya kuhifadhi maji ya mvua. Aliongeza kua, “Nilipanda miti sii kwa ajili ya kufanya biashara lakini ni kwa sababu ya kuhifadhi ukijani katika mazingira ya nyumba yangu.” Na pia kuacha kuku, kwa sasa anafuga sungura, samaki, kanga, nguruwe, mbuzi na ngombe.

Kulingana na wataalamu, kulima mazao mbalimbali kunaleta uzalishaji wa vyakula, inasaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, na kutoa bidhaa mbali mbali na huduma ambayo inaimarisha maisha na kipato cha mkulima. Bw. Paulo anasema “Kama unafuga kuku na una bwawa la samaki, unaweza ukaanza kulima bustani ndogo ya mboga ambapo kuku wataweza kupata chakula na masalia ya kuku yanaweza kua chakula cha samaki. Maji kwenye bwawa la samaki huweza kutumika kwa umwagiliaji wa mboga.”

Taarifa hizi zimepatikana kwa kuwezeshwa na Elanco Animal Health.