Zuia malaria wakati wa ujauzito!

| Novemba 20, 2018

Download this story

Tatizo la Malaria wakati wa ujauzito na katika watoto linaendelea kuwepo nchini Zambia na kote barani Afrika. Ugonjwa huu umesabababisha vifo vingi, hasa kwa wanawake wajawazito na watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.

Kulingana na Kituo cha Udhibiti wa Malaria nchini Zambia (The National Malaria Control Center), malaria huua zaidi ya watu milioni moja duniani kila mwaka, wengi wao wakiwa wanaishi Afrika, kusini mwa Sahara. Zaidi ya vituko milioni tatu za malaria huripotiwa katika vituo vya afya duniani kila mwaka. Hii ni mara tano ya maambukizi ya kifua kikuu, UKIMWI, surua na ukoma kwa pamoja. Malaria husababisha kifo kimoja kwa kila vifo vinne vya utotoni barani Afrika. Ugonjwa huu huua mtoto wa Kiafrika kila sekunde 30. Wale wanaonusurika maradhi kali ya malaria huweza kuwa na ulemavu mkuu wa kimwili na kiakili.

Ni jambo la kusitikisha kuwa wanawake wana uwezekano mara nne wa kuugua na mara mbili wa kufariki kutokana na malaria endapo ni wajawazito. Nchini Zambia, asilimia ishirini ya vifo vya wakati wa ujauzito vinatokana na malaria. Wanawake wajawazito na watoto wanaougua malaria huchukua asilimia kubwa ya vitanda hospitalini.

Wataalam wa kiafya hupendekeza mambo kadhaa kuzuia uzambazaji wa malaria. Pendekezo mojawapo ni kutumia nyavu za vitandani zilizotibiwa kwa dawa ya mbu manyumbani. Pendekezo lingine ni kuhakikisha boma na maeneo ya karibu nazo yamepuliziwa dawa. Wanawake wanaoishi katika maeneo yenye malaria wanapaswa kunywa madawa ya kuzuia malaria kila mara wanapokuwa wajawazito ili kujikinga wenyewe na pia mtoto aliye tumboni.

Makala haya yanaangazia tajriba ya Bi. Mirriam Chawila, mwanamke Mzambia ambaye ana mimba ya miezi saba. Yanaonyesha mambo aliyokumbana nayo wakati malaria yalimvamia vikali.

Makala haya ni igizo ndogo lenye misingi ya mahojiano halisi na mwanamke mjamzito na maofisa wa afya. Unaweza kutumia makala haya kama msukumo kutafiti na kuandika makala juu ya mada sawia katika eneo lako. Ama unaweza kuchagua kutoa makala haya katika kituo chako ukitumia waigizaji wa sauti kuwakilisha wazungumzaji. Endapo utafanya hivyo, tafadhali hakikisha unaiambia hadhira yako mwanzoni mwa kipindi kuwa sauti hizo ni za waigizaji na wala si wazungumzaji asilia.

http://scripts.farmradio.fm/sw/radio-resource-packs/package-91-soil-health/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito/