DRC: Wakulima wanaungana pamoja ili kuboresha soko la mahindi yao

July 03, 2019
A translation for this article is available in English French

Henriette Sahengema anatoka katika jengo kubwa la cinderblock akihesehabu malipo mapya kwa furaha akitabasamu katikati ya wakulima kadhaa.

Hii ni mara ya kwanza kupata dola za kimarekani $ 280 katika mikono yake baada ya kuuza mahindi. Akishangaa, anasema, “Ninafurahi kushika fedha nyingi kama mkulima mdogo.”

Bi Sahengema ana umri wa miaka 43. Muuguzi kwa taaluma, amekuwa akilima mahindi kwa kipindi cha miaka saba iliyopita kwenye shamba la hekta 25 huko Rutshuru, jimbo la Kaskazini Kivu la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yeye ni mwanachama wa kikundi cha wakulima Kiwanja, ambacho kilianzisha ushirika miaka mitatu iliyopita ili kuongeza thamani ya mavuno katika soko.

Wakulima walikuwa wakiuza mfuko mmoja wa mahindi wenye kilo 120 kwa dola za kimarekani $ 15. Waliuza kwa madalali wa mazao, ambao waliuza mahindi yao kwa bei ya juu katika masoko ya mijini.

Bi Shahengema anakumbuka kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya masoko ya pamoja mwanzoni. Lakini baada ya msimu wa 2016, wakulima waliamua kukusanya mazao yao. Anasema, “Ilikuwa ni tani 15 za mahindi na tuliihifadhi katika nyumba ya mtu mmoja ili kuuza baadaye.”

Chama cha ushirika kiliamua kuwa kundi la wanachama litatafuta wanunuzi katika masoko ya kikanda. Waliweza kuuza gunia la kilo 120 ya mahindi kwa dola $ 40, zaidi ya mara mbili ya dola $ 15 inayotolewa na wanunuzi wa kati wa ndani. Ushirika hugawanya mapato kulingana na kiasi cha mahindi cha kila mwanachama alichohifadhi.

Bi Shahengema anasema amekuwa akivuna magunia matano au kilo 600 za mahindi kutoka shamba lake la hekta 25, lakini sasa anapata mara mbili au wakati mwingine mara tatu kiasi alichokuwa akipata. Anasema, “Ninajua siri leo: Ni muhimu kuzalisha kwa ubora na wingi na kisha kujiunga na wakulima wengine kuhifadhi na kisha kupata soko zuri pamoja.”

Ushirika wa Masoko unajulikana kama COPROVEPA na una wanachama mia moja ambao huzalisha na kuuza bidhaa za kilimo. Wanayo ghala ili kuhifadhi nafaka zao, ambao wamejenga kwa msaada kutoka kwa mdau wa ndani.

Chama hicho cha Ushirika kina kamati kadhaa za usimamizi: bodi ya usimamizi, kamati ya kuhifadhi, na kamati ya wakulima. Bodi hizi hutekeleza maelekezo yaliyotolewa na wanachama wa wakulima wakati wa mikutano ya jumla, ambayo hufanyika mara mbili kwa mwaka.

Ni wajibu wa kamati moja kutafuta masoko mapya ya kuuza bidhaa zao, na kuweka lengo la kuboresha maisha ya wakulima katika Rutshuru. Chama cha ushirika kinawateja wake ambao ni shirika la chakula duniani na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Mashirika haya mawili hivi karibuni yalinunua mifuko 280 ya mahindi.

Lwanzo Lupeta alilipa dola za marekani $ 5 US kwa kujiunga na chama cha ushirika, akiwa umri wa miaka 38 hajawa hi kujutia uamuzi wake. Tangu 2016, ameongeza mavuno yake katika kikundi mara tatu ili kuuzwa kwa pamoja. Mapato yake yameongezeka mara mbili zaidi.

Kwa muda mrefu, Bwana Lwanzo aliuza mahindi yake kwa wanunuzi wadogo wa ndani. Anakumbuka kwa uchungu, “Niliuza gunia la kilo 120 la mahindi kwa dola $ 10 au $ 15. Kibaya zaidi walikuwa wanunuzi ambao walitumia mbinu za jadi za kupima mahindi.” Walitumia bakuli kubwa ya alumini ili kukadiria uzito, aina ya kipimo ambacho si sahihi na huwaacha wakulima wakihisi kama waliporwa.

Bwana Lwanzo anasema kuwa uuzaji wa pamoja unampa faida kubwa na inaruhusu aweze kulipa kodi na ada za shule kwa urahisi na kununua chakula kwa ajili familia yake.

Sindibuve Fabien ni mwenyekiti wa chama hicho cha ushirika. Anasema kikundi kinapokea maombi kutoka kwa wakulima wanaotaka kujiunga. Changamoto ni kuhakikisha kwamba mazao yote ya mavuno yanaweza kuhifadhiwa kwa ufanisi ili kuepuka hasara, lakini zaidi ya yote kuuza kwa bei nzuri. Wanunuzi wanatafuta linapokuja suala la ubora, na chama cha ushirika wanawafundisha wazalishaji ili kufikia viwango vyao. Bwana Sindibuve anasema, “Tunahakikisha kwamba wakulima wamechambua na kukausha mazao yao vizuri kabla ya kuiweka kwenye makaratasi ya kibanda katika kituo chetu cha jamii.”

Ili kuongeza muda wa kuhifadhi na kulinda mahindi kutokana na kushambuliwa na wadudu, chama cha ushirika hutumia mifuko ya Kuhifadhia yaliyoboreshwa ya Purdue*, pia inajulikana kama mifuko ya PICS. Mfuko huu umetengenezwa ili kuboresha uhifadhi wa nafaka kama mahindi kwa sababu yana tabaka mbili ambayo hupunguza hasara kutoka kwa wadudu waharibifu au hali ya unyevu. Mifuko hii huunda utupu ambao unaua wadudu kwa kuondoa unyevu wanaohitaji ili kuishi.

Kwa mahindi bora, uzoefu mzuri wa kuhifadhi, na uhusiano wa moja kwa moja na watumiaji, chama hiki cha ushirika kinafanya wakulima wa Rutshuru kupata kipato kizuri kutokana na kazi yao ngumu.

*Angalia: Purdue, pia inajulikana kama mifuko ya PICS. Mfuko huu umetengenezwa ili kuboresha uhifadhi wa nafaka kama mahindi kwa sababu yana tabaka mbili ambayo hupunguza hasara kutoka kwa wadudu waharibifu au hali ya unyevu.

Rasilimali hii imetafsiriwa kwa msaada wa shirika hisani la Rockefeller kwa njia ya mpango wake wa uwezeshazaji wa YieldWise.