Tanzania: Wanawake waendelea kupanda maharage pamoja na changamoto ya masuala ya kijinsia

December 03, 2018
A translation for this article is available in French English

Ingawa ni mchana na kuna jua kali, Verantikisi Daniel Kaaya anaonekana akiketi barazani mwake akiwa ameshikilia beseni lake la chuma analotumia kupepeta maharage ili kuondoa uchafu. Anasema,, “Nimekuwa niki lima maharage kwa miaka mingi sana pamoja na kuwepo na changamoto nyingi sana katika shughuli hizi kama mkulima mwanamke, changamoto hizi hazinizuii mimi kulima maharage.”

Bibi. Kaaya anaishi kijiji cha Kikatiti mkoani Arusha, kaskazini mwa nchi ya tanzania. Baadhi ya changamoto wanawake hawa wanazo kumbana nazo ni pamoja na kutopata mbegu na kukosa ushauri wa kitaalamu juu ya uchaguzi wa mbegu, kupanda,kupalilia,kuhifadhi, na mbinu za kuvunia.

Bibi. Kaaya anaongeza kwa kusema, “Kumiliki ardhi, matumizi ya dawa na kufanya maamuzi [juu ya mbinu za kilimo] ni moja kati ya changamoto kubwa tunazo kumbana nazo.”

Juu ya umiliki wa ardhi, Bibi. Kaaya anasema kuwa wanawake wengi katika eneo lake wanamavuno kidogo kwasababu wanalima maharage katika eneo dogo ambalo wamepewa na waume zao na eneo linamilikiwa na mume.

Bibi. Kaaya anasema anajihisi mwenye bahati kwasababu anamiliki ardhi tofauti na wanawae wengine. Anaelezea, “Mume wangu anamiliki shamba lakini anafanya kazi katika kampuni ya utalii, hivyo ananiruhusu kulima jinsi ninayotaka.”

Wanawake pia wanachangamoto kubwa ya kuhangaika kujaribu kupulizia dawa katika mashamba yao kwani wume zao wanafanya shughuli nyinginezo na kushindwa kupata nafasi ya kuwasaidia waume zao. Bi. Kaaya anaelezea: “Huwa ninawaajiri vibarua wanaume kupiga dawa shambani kwangu kwasababu siwezi kubeba bomba zito mgongoni mwangu… lakini ninapokosa vibarua muda mwingine ninalazimika kupiga dawa mwenyewe.”

Bibi. Kaaya anasema wanawake wengi katika eneo hili hawana mamlaka ya kufanya maamuzi juu ya kilimo na hawana nafasi ya kushindana na wanaume. Ijapokuwa Bibi. Kaaya hawezi kufanya maamuzi katika familia yake, ni afadhali kwani baadhi ya muda huwa mume wake anamsikiliza.

Anaelezea, “Huwa ninajadili na mumewangu juu ya zao ninalotaka kupanda, katika eneo gani pamoja ni nini cha kufanya baada ya kuvuna, kuuza au kuhifadhi.”

Honoratha Shirima ni afisa ugani katika eneo hili. Anasema. Kuna umuhimu mkubwa wa kuwapatia mafunzo ya haki za kijinsi wanaume wa eneo hili ili waweze kuwapa wanawake hazi za kufanya maamuzi katika kilimo. Bibi. Shirima anaelezea, “Kama wanawake wangepewa haki ya kumiliki ardhi na kufanya maamuzi, itapelekea kuwa na maenedeleo.”

Grace Vanika ni mkulima wa maharage anayeishi kijiji cha Kikatiti village. Anasema maharage sana sana ni zao linalolimwa na wanawake, lakini changamoto kubwa ni utamaduni unawazuia wanawake kuendelea.

Bibi. Vanika anaongeza kwa kusema, ni vigumu kwa wanawake kuweza kufuata mbinu bora za kilimo cha maharage kwasababu jamii ina mpa mkulima wa kiume haki zote na kumnyima mwanamke haki za kufanya maamuzi.

Anaelezea: “Ijapokuwa wanaume wengi hawalimi Maharage, wanamaamuzi juu ya mauno …. Wanawake katika eneo hili wanapewa maeneo madogo ya kupanda maharage, wanawake wana pewa ekari moja kati ya shamba la ekari mpaka kumi.”

Bibi. Vanika anasema, ingawa wanawake wanatumia eneo dogo wanalopewa kulima maharage, wanaume wanapaswa kuwasaidia wake zao ili kwa pamoja waweze kuzalisha vyema and feed the family.

Bibi. Vanika anasema kuwa, kukabiliana na changamoto hizi, wanawake katika eneo lake wameanzisha kikundi cha wakulima 20 mpaka 25. Kwa kupitia vikundi hivi wataalamu wa kilimo na mashirika yasiyo ya kiserikali yanaweza kuwatembelea kiurahisi na kuwapatia mafunzo

Simulizi hili limeandaliwa na msaada wa USAID New Alliance ICT Extension Challenge Fund, kupitia mfuko wa msaada wa kimataifa wa kilimo Tanzania. Kwa taarifa zaidi juu ya mfuko huu tembelea, please see: https://www.ifad.org/

This story was prepared with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/