Tuzo za Liz Hughes kwa mradi wa Her Farm Radio

| Januari 22, 2019

Download this story

Farm Radio International imeandaa tuzo mpya zinazo tambua vituo vya redio vinavyo gusia masuala ya kijinsi na kupaza sauti za wanawake wa vijijini. Farm Radio International inawaalika vituo vya redio na timu ya uzalishaji vipindi lutuma maombi yao kwaajili ya kushiriki katika tuzo hizi za Liz Hughes.

Liz Hughes alikuwa ni mwanachama wa bodi ya farm radio na pia alikuwa na shauku kubwa katika utangazaji na alikuwa ni bingwa katika masuala ya jinsia. Shirika la Utangazaji la Kanada liliisaidia shirika la farm radio kuandaa mfumo uitwao FAIR journalistic standards, mfumo huu unahimiza usawa na haki, uhakika,uadilifu na Heshima.

Vijiji barani Afrika, nchi za kusini mwa jangwa la sahara, wanawake wanamchango mkubwa katika shughuli za kilimo na jamii kwa ujumla. Lakini wanahatari kubwa ya kukumbwa na janga la njaa, utapiamlo, na afya mbaya, na hawana haki ya kumiliki wala utumiaji wa mali. Ni muhimu kituo cha redio kugusia mahitaji ya wanawake na wanaume pia. Ili wote wanaume na wanawake waweze kunufauka na taarifa zinazotolewa na kuweza kuchangia katika maendeleo ya kijamii. Jifunze zaidi jinsi ya kuweza kuwahudumia wanawake wakulima katika chanzo hiki cha taarifa kwa waandishi wa habari

Kituo chochote cha redio barani afrika kinaweza kutuma maombi yake kupata tuzo hizi. Wanapaswa kutuma kipindi chochote cha redio ambacho wanaona kuwa waligusia masuala ya kijinsia kwa wanawake wa vijijini. Kituo kimoja cha redio kinaweza kutuma maombi mbali mbali kama kina vipindi mabli mbali vyenye vigezo tajwa.

Watuma maombi wanalazimika kujaza fomu ya maombi na kuambatanisha rekodi katima mfumo wa MP3, fomu na rekodi zote zitumwe kwenda radio@farmradio.org. Tafadhali kichwa cha taarifa kiwe: Liz Hughes Award for Her Farm Radio

Maombi yatapokelewa katika lugha ya kingereza, French, Amharic, na Swahili, na Hausa. Rekodi utakayoambatanisha inaweza kuwa imerekodiwa kwa lugha ya mahali husika.

Mwisho wa kutuma maombi ni mwezi wa pili 17.

Timu itakyo shinda itapokea cheti na kiasi cha dola za Kikanda 1,000 kama tuzo kutambua kazi zao bora.

Pakua fomu ya maombi hapa.