Kenya: Wakulima wa maembe hutumia mifuko ya chupa ya plastiki kukabili nzi wa matunda

| Disemba 10, 2019

Download this story

Shamba la Bw. Josiah Mwangi limejaa miti ya maembe. Ukiliangalia kwa umbali, miti inaonekana kuunda dari, yenye visehemu vya kijani kibichi kilichonyooka hadi kwenye upeo wa macho. Kwenye shamba, baba wa watoto watano anatembea kwa hatua za vishindo kwenye majani makavu ya maembe yalioanguka.

Kwenye mkono wake wa kushoto, Bw. Mwangi ameshikilia chupa ya lita moja ya plastiki yenye matundu yaliyotobolewa kando kando kuwezesha nzi kuingia, wakivutiwa na chambo iliyo ndani ya chupaa. Ataining’iniza chupa kwenye mti mmoja wa maembe kutega inzi wa matunda, mdudu anayeshambulia matunda ya maembe na anahusika kwa hasara ya hadi asilimia 60 baada ya mavuno. Anasema, “Nzi wa matunda ni wadogo, lakinini wanasababisha uharibifu mkubwa.”

Bw. Mwangi anaibukia kijiji cha Kabiti eneo la kati ya Kenya Kaunti ya Murang’a. Hapa Kambiti, maembe huanza kuiva mwezi wa Novemba. Kama wakulima wengine katika kijiji chake, Bw. Mwangi amo kwenye shughuli ya kuweka mitego kuzuia inzi wa matunda kwenye bustani lake.

Inzi wa matunda huharibu matunda yanayoiva wakati nzi waliokomaa wanapotaga mayai yao ndani ya tunda. Mayai huanguliwa kati ya siku 2 – 4 na mdudu hujilisha kwa tunda na kusababisha uozo kwa tunda.

Bw. Mwangi alikuwa akikuza maindi kama zao la kujipatia fedha lakini akabadilisha hadi kilimo cha maembe kwa sababu ya mvua isiyotabirika katika eneo lake. Lakini 2013 ilikuwa ya machungu: Alipoteza karibia asilimia 80 ya ekari yake mbili ya maembe yaliyokuwa yakiiva kutokana na inzi wa matunda.

Anasema, “Kilimo cha maembe ni mojawapo wa mazao ya kutegemewa ya kuleta mapato, Lakini bado tungali na pigo la shambulizi la wadudu inayoweza kuharibu mavuno yote katika msimu.”

Kufuatia mafunzo juu ya ushughulikiaji wadudu iliyofanywa na kampuni ya ushauri ya Farmtrack, Bw. Mwangi na wakulima wengine walijifundisha jinsi ya kutumia kopo linalofanana na jagi lenye matundu yaliyotobolewa kando kando kama mtego wa inzi wa matunda.

Bw. Mwangi anasema: “Singeamini hili lingefanya kazi, lakini naweza kulishuhudia kwa sasa. Kupitia kwa mitego ya inzi wa matunda, naweza kukuhakikishia kuwa nimeona upungufu mkubwa kwa hasara ya matunda ya maembe kila msimu.”

Farmtrack waliwafundisha wakulima kutumia pheromones/kemikali inayotoka kwa wanyama inayoadhiri viumbe wengine. Pheromones hufanya kazi sawa na homoni, na mitego huitumia kama chambo kuvutia inzi wa matunda wa kiume ndani ya kopo ili kuzalisha wa kike. Inzi wa matunda wa kiume hutegwa ndani na kufa kwa sababu mtego pia huwa una dawa ya wadudu. Kwa hivyo mtego husadia kupunguza idadi ya wadudu kwa kuhitilafia kuzaana.

Wakulima wanaweza kununua chambo iliyotengenezwa kibiashara madukani kwa shilingi 300 ya Kenya (kama dolla 3 za kimarekani) na kopo kwa shilingi 100 ya Kenya (kama dolla 1 ya Kimarekani). Kupunguza gharama, wakulima wanatumia chupa za plastiki zinazopatikana tayari. Wakulima wanatoboa matundu kwenye chupa badala ya kununua makopo ya kutega inzi.

Samson Ndauti ni mkulima wa maembe anayeishi katika kijiji cha Kambiti na alifundishwa na Farmtrack. Anasema: “Wakulima kwa haraka wamelichukua wazo na sasa wanajitengenezea mitego hii wenyewe. Mitego inaning’inizwa kwenye miti ya maembe, chambo ikitumika kwa miezi mitatu ya msimu wa uvunaji wa matunda ya maembe.”

Hapa, maembe hukuzwa kwa msimu mmoja unaokwenda kutoka Novemba hadi Februari au Machi. Bw. Ndauti anasema kuwa wakulima wanafaa kuweka mitego ya inzi wa matunda mapema hadi mwisho wa Novemba.
Aelezea: “Hii inahakikisha kuwa mkulima hagharamiki zaidi kwa ununuzi wa chambo. Mmoja hununua chambo mara moja kila msimu. Hata hivyo, wale ambao hupanda maembe aina mbalimbali yaliyochelewa kukomaa wafaa kutumia chambo kwa Zaidi ya miezi mitatu.”

Mary Wangui Ni mkulima mwingine wa maembe mashinani. Mama wa umri wa miaka 41 na mama wa watoto wanne asema kuwa, tangu aanze kutumia uvumbuzi rahisi wa chupa za plastiki kukabiliana na inzi wa matunda amepata ufanisi mkubwa kupunguza hasara baada ya mavuno.

Anasema: “Wakati mmoja karibia nipoteze mavuno ya msimu wote kutokana na vamizi la inzi wa matunda kwenye shamba langu la ekari moja. Hata hivyo, mitego ya inzi wa matunda, hasa tunapotumia vifaa vinavyopatikana mumu humu kama vile plastiki, imetusaidia kwenye vita.”

Raslimali hii imefadhiliwa na wakfu wa Rockefeller Foundation kupitia mpango wake wa YieldWise.