Tanzania: Wakulima kuanza kuzalisha mihogo kama zao la kibiashara kutokana na ongezeko la hitaji

August 13, 2018
Une traduction pour cet article est disponible en Français Anglais

Ni muda wa jioni lakini Joram Mikanda bado yuko shambani kwake, akiangalia kama mihogo yake imekomaa na iko tayari kwa kuvunwa. Bw. Mikanda ni mkulima mzoefu wa mihogo. Anaelezea,“Nimekuwa nikizalisha mihogo tangu miaka ya 1990s…. Kwanzia mwaka huo mpaka leo nimeweka nguvu zangu katika kuzalisha mihogo.”

Bw. Mikanda anaishi kijiji cha Kitahana mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania, ambapo mihogo inahitajika sana na viwanda vya kusindika pombe na nchi za jirani.

Kitamaduni, watu waishio maeneo haya mihogo inayozalishwa hawapendelei sana mihogo; wanapendelea unga wa mahindi kutengeneza kupika chaula cha asili kijulikanajo kama ugali. Lakini ongezeko la uhtaji wa mihogo imepelekea uhitaji mkubwa wa zao hili masokoni, na wakulima wengi wameanza kuzalisha mihogo kama zao la kibiashara. Wakulima wanasafirisha mihogo yao Rwanda, Jamuhuri ya muungano wa kidemokarasia ya Congo, na Burundi.

Bw. Mikanda anaelezea: “Ninauza mihogo mibichi soko la ndani na ninasafirisha mihogo iliyokaushwa nje ya nchi …. Kwa muda huo [mika ya 1990], Nilikuwa nikisafirisha [mihogo] nchini Burundi kwa baisikeli ambapo niliuza kwa shilingi 20 mpaka 50 [sawa na dola 0.01 mpaka dola 0.02] kwa kilo moja, [lakini] ni vigumu na hatari kuendesha baisikeli njia za porini.”

Bw. Mikanda anasema mashirika yasiyo ya kiserikali na maafisa ugani wanawahimiza wakulima kupanda mbegu bora za mihogo kwasababu zinahitajika zaidi katika kambi za wakimbizi na nchi za jirani.
Christopher Chubwa ni mkulima katika kijiji cha Kitahana, alianza kulima mihogo tangu mwaka 2000. Sasa anaweza kuhudumia familia yake kwa kipato anachokipata. Anasema, “Ninauza mihogo mibichi na mikavu katika kambi ya wakimbizi ya Nduta. Pia ninasafirisha mihogogo mikavu kupeleka Rwanda, Burundi, nchi ya jamuhuri ya muungano wa Congo na Uganda.”

Bw. Chubwa anasema, katika eneo lake, ni kama mgodi wa madini. Wakulima zaidi na zaidi wanategemea kipato kwa kuuza mihogo. Kulingana na Bw. Chubwa, wakulima katika maeneo haya wanataka kuanza kuzalisha unga wa mihogo na vyakula vya mifugo kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi.

Anasema, “Kwa wazalishaji wa mihogo, tumeunda kikundi cha watu 25. Tumejenga jengo ambapo tunataka [kuanza] kufanya usindikaji wa mihogo.”

Victor Kabunga ni mtaalamu wa kilimoi wilayani Kibondo aliyefanyakazi kwa muda wa miaka 9, katika maeneo mengi ikiwemo kijiji cha Kitahana. Mara nyingi huwa natembelea mashamba ya wakulima wa mihogo kuona namna wanavyofanya na kuwapa ushauri.

Bw. Kabunga anasema, “Ninawaeleimisha wakulima jinsi ya kupanda mihogo kitaalamu ikiwemo kupanda kwa nafasi na kuchagua vipando bora vya mihogo.”

Bw. Kabunga anaongeza kwa kusema wakulima na wafanyabiashara wanapata vibali vya kuuza mihogo kutoka kwa waziri wa kilimo. Wakitaka kuuza mihogo katika mikoa mingine nje ya kibondo Tanzania, wanapata kibali afisa wilaya wa kibondo.

Bw. Mikanda anasema maisha ya baadae kwa kilimo cha mihogo ni nzuri. Anaongeza, “Malengo yangu ni kudafirisha mihogo nje ya africa, na ndio maana tunataka kuanzisha kiwanda ambacho tutakuwa tukisindika mihogo.”

Anasema, “Tunawaomba serikali kuboresha miundo mbinu mkoani kigoma ambayo itatusaidia kurahisisha usafirishaji wa mihigo nje ya mkoa na nchi za jirani.”

Bw. Mikanda anasema kipato kutoka katika uzalishaji wa mihogo kimeboresha maisha yake,. Anaelezea: “Msimu uliopita, Nilisafirisha tani 20 za mihogo mikavu na niliuza kwa shilingi 500 [sawa na dola 0.22] kwa kilo. Nilitumia hela hii kulipa ada ya watoto na matumizi mengine ya nyumbani.”

Kazi hii imefanyika kwa msaada wa shirika la AGRA, the Alliance for a Green Revolution in Africa, kama sehemu ya mradi, “Mradi shirikishi wa kuongeza kipato na kuongeza chakula na kuboresha maisha ya wakulima wadogowadogo magharibi mwa Tanzania mkoani Kigoma.” Madhuni yaliyomo katika simulizi hili hayahusiki moja kwa moja na shirika la AGRA au shirika lolote.